25.4 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Wabunge watakiwa kuzingatia umuhimu wa mabadiliko ya Sheria ya Habari

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Wabunge wameombwa kutumia Mamlaka yao vizuri katika kupitisha Mswada wa marekebisho ya sheria ya Huduma za vyombo vya habari ya mwaka 2016 ambao unatarajiwa kupelekwa Bungeni Januari 2023 hatua itakayosaidia sekta ya habari kufanya kazi katika mazingira rafiki.

Ombi hilo limetolewa Desemba 29, 2022 na Mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa habari wa kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya pamoja na uhalifu nchini Tanzania (OJADACT) Edwin Soko wakati akizungumza na Waandishi wa Habari.

Amesema kati ya Sheria ambazo zinakwaza sekta ya habari siyo hiyo peke yake zipo nyingi ikiwemo sheria ya takwimu ya mwaka 2015,sheria ya makosa ya kimtandao ya mwaka 2016 hivyo bunge liwe na desturi ya kupitia sheria hizo ili kuweza kupata sheria ambayo itakuwa rafiki katika sekta ya habari hapa nchini.

”Mswada huu ulipitiwa kweye mikutano mbalimbali ya wadau namimi nilipata bahati ya kuwa miongoni mwa watu waliotoa mapendekezo kupitia taasisi za uchechemzi juu ya suala la kupata habari ambapo tulitoa mapendekezo vizuri kwakushirikiana na Serikali,” amesema Soko.

Soko ameeleza kuwa marekebisho hayo yatawasaidia waandishi wa habari kufanya kazi zao kwa uhuru sanjari na taifa kubadilika kidemokrasia na kupelekea kupata maendeleo katika nyanja mbalimbali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles