32.2 C
Dar es Salaam
Monday, January 30, 2023

Contact us: [email protected]

TRA Kariakoo yazindua Kampeni ya Kuelimisha Wanunuzi Umuhimu wa Kudai Risiti

Na Koku David, Mtanzania Digital

MENEJA wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mkoa wa Kikodi Kariakoo, Alex Katundu amezindua kampeni ya Twende Nao Tukawaelimishe yenye lengo la kuwaelimisha wanunuzi kuhusu umuhimu wa kudai risiti za kielektroniki za EFD kila wanaponunua bidhaa katika eneo la kibiashara la Kariakoo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Desemba 29, 2022 baada uzinduzi huo wakati akiwapa elimu ya umuhimu wa kudai risiti kwa wanunuzi waliokutwa wamenunua bidhaa bila kudai risiti, Katundu alisema elimu ya kodi imekuwa ikitolewa mara kwa mara kwa wafanyabiashara pekee jambo ambalo ualakuwa likisababisha wanunuzi wengi kusahau wajibu wao wa kudai risiti.  

“Mara nyingi tumekuwa tukitoa elimu kwa wafanyabiashara kuhusu matumizi sahihi ya mashine za kutolea risiti za EFD lakini sasa hivi tumekuja na mkakati maalumu wa kuwaelimisha wanunuzi juu ya haki yao ya kudai risiti kila wanapofanya manunuzi,” alisema Katundu.  

Alisema katika kutekeleza zoezi hilo, watakuwa wakikusanya wanunuzi watakaokuwa wamenunua bidhaa mbalimbali bila kuwa na risiti na kupelekwa katika ofisi ya TRA Kariakoo, Dar es Salaam kwa ajili ya kuwaelimisha.  

“Kwakuwa wanunuzi hawa wanakutwa katika maeneo mbalimbali ya Kariakoo, hivyo zoezi hili litafanyika kwa kuwakusanya wote wanaokutwa wamenunua bidhaa lakini hawana risiti na wataletwa hapa ofisini kwa ajili ya kuwaelimisha na kuwaomba wawe mabalozi kwa wengine wenye tabia ya kutokudai risiti,” alisema Katundu.

Alisema elimu hiyo itakuwa ikitolewa bure kwa kuwaeleza wanunuzi umuhimu wa kudai risiti ili kuepuka adhabu ya faini ya Sh 30,000 hadi Sh milioni 1.5.

Kwa upande wake, Elizabeth Kimaro ambaye ni mnunuzi wa bidhaa Kariakoo, alitoa wito kwa wanunuzi wenzake wenye tabia ya kutokudai risiti kutumia haki na wajibu wao wa kudai risiti kwa maendeleo ya Taifa.

- Advertisement -

Related Articles

2 COMMENTS

  1. Badala ya kuwakamata wanunuzi wasiodai risiti kwanini wasiwakamate wauzaji nao na kuwapeleka ofisini?
    Huu ni ubaguzi au TRA imeshindwa kuwadhibiti wauzaji na akwa hivyo wanawabana wanunuzi
    Pia TRA imeshindwa kuwabana wamachinga ambao wanauza bidhaa zaidi ya shilingi 100,000. Na kwa hiyo TRA imewasamehe wamachinga wasitoe risiti. Hii ikoje? Ni sheria gani?

  2. Nyie TRA Kariakoo hebu jaribuni kutembelea duka la Azam lililo karibu yenu. Hapo kuna biashara za mamilioni bila ya risiti. Je mmechukua hatua gani? Halafu mnataka kuwabana wanunuzi. Acheni unafiki

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles