29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 28, 2024

Contact us: [email protected]

Wabunge Ethiopia wamchagua rais mwanamke

                          Addis Ababa, Ethiopia
Wabunge nchini Ethiopia wamemchagua Sahle-Work Zewde, kuwa rais wa kwanza mwanamke baada ya aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Mulatu Teshome, kujiuzulu ghafla leo.

Sahle-Work ni mwanadiplomasia mwenye uzoefu ambaye sasa amekuwa kiongozi wa kipekee mkuu mwanamke barani Afrika.

Kuchaguliwa kwake katika wadhifa huo, kunajiri wiki moja baada Waziri Mkuu, Abiy Ahmed, kuliteua baraza la mawaziri ambapo nyadhifa nusu katika baraza hilo zimewaangukia wanawake.

Katika hotuba yake ya kukubali wadhifa huo, Rais Sahle-Work, amezungumza kuhusu umuhimu wa kudumisha amani.

Rais Sahle-Work amewahi kuwa Balozi wa Ethiopia nchini Senegal na Djibouti na amewahi kushika nyadhifa kadhaa katika Umoja wa Mataifa ikiwamo Mkuu wa Kujenga Amani katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles