29.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

WABUNGE CUF LIPUMBA WAUNDA UMOJA WAO

Na MAREGESI PAUL -DODOMA

WABUNGE wa Chama cha Wananchi (CUF) wameunda uongozi wao ndani ya Bunge.

Uongozi huo ulitangazwa jana na Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson, muda mfupi baada ya kipindi cha maswali na majibu.

Kwa mujibu wa Naibu Spika, uongozi huo uliwasilishwa ofisini kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai na Mbunge wa Kaliua, Magdallena Sakaya (CUF).

Akitangaza uongozi huo jana, Naibu Spika alisema wabunge hao wa CUF watakuwa wakiongozwa na Mwenyekiti ambaye ni Mbunge wa Mtwara Mjini, Maftah Nachuma na Katibu wake atakuwa Mbunge wa Viti Maalum, Rukia Ahmed.

Dk. Tulia alimtaja Mbunge wa Kinondoni, Maulid Mtulia, kuwa ndiye Mnadhim Mkuu wa wabunge hao wakati Sonia Magogo alichaguliwa kuwa mweka hazina wa wabunge hao.

Hata hivyo, Mbunge wa Malindi, Ally Salehe (CUF), alionyesha kutoridhishwa na uongozi huo kwa kile alichosema chama chao kilishafanya uteuzi wa wabunge wengine kushika nafasi hizo.

“Mheshimiwa Naibu Spika, hapa umetutangazia juu ya uongozi mpya wa CUF wakati sisi tunajua kuna viongozi tuliwachagua kwa kura za wabunge 42.

“Sasa nataka nikuulize, hivi ni nani katika chama anayeruhusiwa kuchagua viongozi?” alihoji Saleh.

Akijibu hoja hiyo, Naibu Spika alisema anachojua yeye ni kwamba  viongozi wa CUF waliochaguliwa ni wale waliopeleka majina yao kwa Spika baada ya uchaguzi kufanyika na kwamba kama kuna uongozi mwingine, yeye hautambui.

“Bungeni kuna viongozi wa kambi ya upinzani, lakini kila chama kina viongozi wake. Hawa niliowataja  ndiyo viongozi waliochaguliwa na wabunge wa CUF na majina yao kuwasilishwa kwa Spika.

“Ila  kama kuna majina mengine, mimi siyajui ingawa hoja yako inaonyesha katika CUF kuna pande mbili zinazovutana,” alisema Dk. Tulia.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles