27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

‘MALARIA, UKIMWI TISHIO UHAI WA BINADAMU’

Na MWANDISHI WETU -MWANZA

UTAFITI mpya uliofanywa na Taasisi ya Taifa Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu   (NIMR) umebaini kwamba magonjwa ya Malaria, Ukimwi, Moyo, Mfumo wa Upumuaji   na Upungufu wa Damu yanayongoza kwa kusababisha vifo   hospitalini.

Utafiti huo  ulifanyika mwaka jana kwa kutumia takwimu za kuanzia mwaka 2006 hadi 2015 katika hospitali 39 nchini ambazo ni pamoja na hospitali ya taifa, hospitali za kanda na hospitali za mikoa na wilaya.

Kwa mujibu wa utafiti huo,  vifo vya ajali vimeongezeka kwa asilimia 16, saratani asilimia 24, kiharusi asilimia 27 na kisukari asilimia 11.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Dk. Leonard Subi alikuwa akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza     kwenye uwasilishaji wa matokeo ya utafiti huo katika mikoa ya Kanda ya Ziwa   na Kanda ya Magharibi jana.

Alisema hatua madhubuti zinapaswa kuchukuliwa kwa kutumia utafiti huo kudhibiti vifo hivyo.

Mtafiti Mkuu Kiongozi kutoka NIMR, Dk. Leonard Mboera, alisema utafiti huo pia ulilenga kuangalia upatikanaji wa takwimu za vifo katika hospitali nchini   ambako ilibainika kuwapo changamoto katika ukusanyaji, uchanganuzi na matumizi ya takwimu katika hospitali.

Taasisi ya NIMR ilifanya utafiti kubaini sababu na vyanzo vya vifo katika hospitali nchini na kubaini kwamba malaria unaongoza kwa kusababisha vifo kwa asilimia 12.8, mfumo wa upumuaji kwa asilimia 10.1, Ukimwi asilimia 8.0, upungufu wa damu asilimia 7.8, magonjwa ya moyo na mfumo wa damu asilimia 6.3.

Katika utafiti huo imebainika mikoa ya Dar es salaam, Mwanza na Morogoro inaongoza kwa vifo katika hospitali nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles