22.8 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

NGELEJA AHOJIWA KWA DCI, MGODI KUFUNGULIWA

PATRICIA KIMELEMETA Na ASHA BANI -DAR ES SALAAM

MBUNGE wa Sengerema, Wiliam Ngeleja (CCM), amehojiwa kwenye ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai (DCI) kuhusu   kuhusika kwake kwenye suala la madini.

Ngeleja ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini katika Serikali ya awamu ya nne, amehojiwa baada ya kutajwa kwenye ripoti za Kamati ya Bunge kuhusu suala la   almasi na Tanzanite.

Mbunge huyo aliwasili kwenye Ofisi ya DCI   Dar es Salaam jana saa nne asubuhi ambako alihojiwa kwa   saa tatu.

Baada ya kutoka kwenye mahojiano hayo kundi la waandishi wa habari lilipomfuta kutaka kujua mahojiano yao yalijikita kwenye nini mbunge huyo hakuwa tayari kueleza.

“Nimefika hapa saa 4.00 na sasa hivi ndiyo natoka (saa 6:30) angalieni saa zenu. Polisi waangalieni hawa wanataka kuniteka,” alisema Ngeleja huku akicheka na kupanda gari na kuondoka.

Mgodi wa Mwadui

Wakati huohuo, Kamishna wa Nishati na Madini, Benjamin Mchwampaka alisema   tayari mazungumzo yamefanyika kati ya serikali na uongozi wa mgodi wa Mwadui.

Akizungumza na MTANZANIA jana, alisema wanaendelea na vikao kuhusu lililotoke,a la uongozi kufunga mgodi ingawa wamekubaliana kuufungua na kuanza kazi kesho.

Alisema tayari Mkuu wa Mkoa  Shinyanga, Zainab Telack, amefanya kikao na  uongozi na wamekubaliana kuufungua kuanza kazi mara moja.

“Tayari walishazima mitambo yao na hadi kuwasha tena itachukua muda hivyo nafikiri keshokutwa mitambo itakua imewaka tayari kwa kuanza kazi.

“Mkuu wa mkoa amezungumza  nao na wizara pia, hivyo viongozi wanajipanga upya na kuendelea na kazi zao…haina shida watarudi kufanya kazi nadhani hakuna madhara kwa wafanyakazi kwa sasa,’’alisema Mchwampaka.

Juz,  uongozi wa Kampuni ya Williamson Diamonds Limited (WDL) ulisimamisha  kwa muda uzalishaji katika mgodi huo.

]Hivi karibuni  wafanyakazi wawili wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere  (JNIA) walikamata mzigo wenye madini ya almasi yenye uzito wa kilo 29, dakika tano kabla ya ndege kuondoka huku yakiwa yameandikwa yana kilo 14.3.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles