JERUSALEM, ISRAEL
WABUNGE wa vyama vya kisiasa vya Kiarabu katika Bunge la Israel wamemuunga mkono mkuu wa zamani wa jeshi, Benny Gantz anaegombea wadhifa wa waziri mkuu, na kumuongezea uwezekano wa kumshinda kiongozi aliye madarakani Benjamin Netanyahu.
Hatua hiyo ya kihistoria ni ishara ya dharau kwa Netanyahau ambaye anashutumiwa kuchochea chuki dhidi ya Waarabu wakati ya kampeni yake ya kugombea tena uwaziri mkuu.
Hii ni mara ya kwanza katika kipindi cha miongo mitatu kwa vyama vya Kiarabu kumuunga mkono mgombea wa wadhifa wa waziri mkuu.
Uamuzi umebaki kwa Rais wa Israel, Reuven Rivlin kuamua ni mgombea yupi wakupewa nafasi ya kuunda serikali ya mseto na kuongoza kama waziri mkuu.
Gantz na Netanyahu wote wawili wamekosa wingi wa viti katika bunge lenye viti 120. Lakini kuungwa mkono na vyama vya Kiarabu, huenda kukamsaidia Gantz.
Muungano wa vyama vya waarabu ambavyo vinamuunga mkono Gantz ni miongoni vile vilivyo katika orodha ya vitakavyounda serikali ya mseto ambavyo vilipata nafasi ya tatu.
Katika uchaguzi uliopita kiongozi huyo wa Israeli Netanyahu alikuwa akichuana kwa karibu na Gantz, na wawili hao sasa wanawania kuunda serikali ya mseto.
Hii ni mara ya kwanza tangu mwaka 1992 kwa kikundi cha wanasiasa wa kiarabu nchini Israeli kumuidhinisha waziri mkuu.
Uchaguzi mkuu huu ulikuwa ni wa pili wa mwaka wa Israeli baada ya ule wa kwanza wa mwezi April ambapo mazungumzo ya muungano yalivunjika na hivyo kuitishwa uchaguzi mwingine.
Akikabiliwa na mkwamo mwingine wa kisiasa , Rais Reuven Rivlin amependekeza kuwepo kwa serikali mpya itakayojumuisha miungano ya yote ule wa Blue wa Gantz na ule wa White pamoja na chama cha wazri mkuu Netanyahu cha Likud.
Rais Rivlin amekwishasema kuwa atafanya kila liwezekanalo kuepuka uchaguzi mkuu wa tatu nchini Israeli mwaka huu.
Aymen Odeh, kiongozi wa mungano, amemuambia Rivlin kwamba kipaumbele cha muungano wao ni kumzuia Netanyahu kuongoza kwa muhula mwingine.
Muungano huo wa vyama vya kiarabu una viti 13 bungeni .
Gantz aliidhinishwa na wabunge wote 13 , lakini bado atahitaji viti 61 vinavyohitajika kupata wingi wa viti katika bunge lenye viti 120.
Huu ni mchakato muhimu wa mamlaka ya kisiasa kwa raia wa Palestina ndani ya Israel
Rais Rivlin anashauriana na viongozi wa chama kuhusu ni nani ambaye atamuomba kuongoza nchi baada ya matokeo ya uchaguzi wa wiki iliyopita ambao hayakutoa matokeo kamili .
Uungaji mkono wao hautampa wingi wa viti, Benny Gantz na muungano wa Blue & White , lakini utamuinua katika mazungumzo kuhusu ni nani atapata nafasi ya kwanza ya kuunda serikali.