23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Waangalizi Umoja wa Ulaya wawasili

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

 

UJUMBE wa waangalizi 34 wa uchaguzi kutoka Umoja wa Ulaya (EU), wamewasili Dar es Salaam kwa ajili ya kufuatilia mwenendo wa uchaguzi mkuu.

Waangalizi  hao wanaungana na kundi kuu la EU EOM la watathmini wa uchaguzi  ambao waliwasili Septemba 11, mwaka huu.

Msafara wa  EU EOM nchini Tanzania, utaongozwa na Mbunge wa Bunge la Ulaya kutoka nchini Uholanzi, Judith Sargentini.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari mjini Dar es Salaam jana na Ofisa Habari wa umoja huo hapa nchini, Sarah Fradgley ilisema ujumbe huo baada ya kupata maelezo kwa siku mbili jijini Dar es Salaam yanayohusu mchakato mzima wa uchaguzi, waangalizi hao watasambazwa mikoa yote.

“Waangalizi hawa watasambazwa makundi ya watu wawili wawili, jukumu lao kwa wiki sita zijazo ni kuangalia maandalizi ya uchaguzi, kampeni na kazi ya utendaji wa mamlaka husika.

“Wataangalia upigaji kura na kuhesabiwa, uorodheshwaji wa matokeo na namna ya kushughulikia  malalamiko na rufaa zinazoweza kujitokeza.

“Waangalizi wetu watakutana na maofisa wa uchaguzi, wagombea na wawakilishi wa asasi za kiraia na watatuma ripoti ya  watakayoyaona kwa kundi kuu Dar es Salaam, ili tathmini ya kina na isiyo na upendeleo iweze kufanyika,”ilisema taarifa hiyo.

EU EOM, imetumwa baada ya kupata mwaliko kutoka Serikali ya Tanzania,Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC).

Tarifa hiyo, ilisema jukumu la ujumbe huo, ni kuangalia masuala yote ya mchakato wa uchaguzi na kutathmini kama uchaguzi unazingatia misimamo ya kimataifa na ya kikanda kuhusu chaguzi za kidemokrasia.

Mwangalizi mkuu, Sargentini, atawasili nchini keshokutwa na atakutana na waandishi wa habari Septemba 30, mwaka

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles