Watu barani Afrika leo Mai 25, 2021 wanaadhimisha sherehe ya siku ya Afrika.
Sherehe hizo zinazoadhimishwa kila mwaka ni ukumbusho wa siku ambapo Shirika la Umoja wa Afrika (OAU), ambalo sasa ni Muungano wa Afrika ulioanzishwa mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa, mwaka 1963.
Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa anatarajiwa kuzindua sanamu ya Nehanda Charwe, maarufu Mbuya Nehanda, ambaye aliongoza mapinduzi ya mwaka ya 1800.
Muungano wa Afrika umekuwa ukiweka taaarifa mtandaoni dondoo za kuvutia kuhusu nchi 55 za wanachama wake.
Muungano huo nchini Cameroon uliangazia juhudi za mwanamume mmoja mwenye umri wa makamo ambaye ameboresha huduma za afya nchini humo.
Katika ujumbe wake, Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesisitiza haja ya nchi za Afrika kudhibiti uhuru wao.
“Kama mataifa ya Afrika, tunataka kujisaidia na wala sio kuambiwa ni kitu gani kizuri kwetu, kanuni ya hakuna chochote kinachotuhusu kitakachojadiliwa bila sisi inapaswa kutumika, “aliandika Rais Ramaphosa.