27.7 C
Dar es Salaam
Saturday, June 10, 2023

Contact us: [email protected]

Karia azionya klabu zinazodaiwa na wachezaji

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania(TFF), Wallace Karia, ameziona klabu za Ligi Kuu Tanzania Bara zinazodaiwa na wachezaji kuwa hata zikitwaa ubingwa msimu ujao hazitashiriki ligi hiyo.

Karia amesema hayo, leo Jumanne Mei 25, 2021 katika hafla ya utiaji saini wa mkataba wa haki za matangazo ya ligi na kampuni ya Azam Media,jijini Dar es Salaam.

Amesema wanataka kuzingatia kanuni ya leseni ya klabu kuanzia msimu ujao na hakuna kuchekeana.

“Sitanii kudaiwa ni jambo hata ukishinda ubingwa, kama unadaiwa na wachezaji huwezi kushiriki Ligi msimu ujao, tunataka kuzingatia kanuni,” amesema Karia.

Amefafanua kuwa kudaiwa na mchezaji ni kwenda kinyume na sheria ya leseni ya klabu, hivyo watafanya utaratibu wa kuhakikisha klabu zina watu wenye sifa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,409FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles