23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Airtel Money yazindua “Airtel Money tunakuunganisha na dunia”

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Kampuni ya simu za mikononi ya Airtel Tanzania kupitia huduma yake ya Airtel Money imezindua kampeni maalum itakayojulikana kama ‘’Airtel Money Tunakuunganisha na Dunia’ ambapo itawawezesha wateja wote wa Airtel Money kupokea fedha kutoka nchi Zaidi ya 200 duniani moja kwa moja kupitia akaunti zao za Airtel Money.

Mkurugenzi wa huduma za Airtel Money Isack Nchunda (kushoto) akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati akizindua kampeni maalum itakayojulikana kama ‘’Airtel Money Tunakuunganisha na Dunia’ ambapo itawawezesha wateja wote wa Airtel Money kupokea fedha kutoka nchi Zaidi ya 200 duniani moja kwa moja kupitia akaunti zao za Airtel Money. Kulia ni Meneja Uhusiano Tanzanai Airtel Jackson Mmbando.

Akizungumza jijiji Dar es Salaam leo Mei 25, 2021 wakati wa kuitangaza kampeni hiyo, Mkurugenzi wa Airtel Money, Isack Nchunda amesema huduma hiyo ya kupokea fedha kutoka nchi zaidi ya 200 itajulikana kama Airtel Money Tunakuunganisha na Dunia na kwamba hakuna mipaka wala changamoto ya kupokea fedha kutoka nje ya nchi ukiwa na Airtel Money sasa.

“Huduma hii ni inadhihirisha dhamira yetu ya kuendelea kushirikiana na serikali ili kuleta suluhisho la huduma za kifedha hapa nchini ili kuwafikia Watanzania wengi ambao bado hawajafikiwa na huduma za kibenki. Tunaelewa ya kwamba tunao ndugu, jamaa na marafiki walio nje ya nchi ambao wangependa kutuma fedha kwa ndugu zao watanzania lakini wanakumbana na vikwazo kutokana na hatua nyingi zinazotakiwa wakati wa kutuma fedha nje ya nchi. Airtel Money imekuja na suluhisho, mteja wa Airtel Money anatakiwa kuwa na laini ya simu ya Airtel ambayo imesajiliwa tu,” amesema Nchunda.

Nchunda ameongeza kuwa Airtel Money Tunakuunganisha na Dunia itaboresha uchumi shirikishi kati ya familia na marafiki waliopo nje ya nchi kwa kuwa itaongeza uhuru wa kuchangua njia rahisi na ya haraka pale inapohitaji kupokea fedha au kwa wanaotaka kutuma fedha hapa nchini kwa haraka, huku sisi Airtel tukiwa tumejipanga kikamilifu kuendelea kutoa huduma nafuu, salama, haraka bila mipaka.

Nchunda amezitaja baadhi ya nchi ambazo mteja wa Airtel Money ataweza kupokea fedha moja kwa moja kwenye akaunti yake ya Airtel Money ni pamoja na Marekani, Uingereza, Ujerumani, Uswizi, Swedeni, Uholanzi, Italia, Norway pamoja na nchi zote za Afrika Mashariki.

“Mnamo mwishoni mwa mwaka jana, Airtel kwa kushirikiana na WorldRemit, ambayo ni kampuni ya kimataifa ya malipo walizindua mfumo huu wa malipo kwa kuwawezesha wateja wa Airtel Money kupokea fedha moja kwa moja kwenye akaunti zao za Airtel Money kwa nchi Zaidi ya 50. Huu ni muendelezo wa kuhakikisha wateja wetu wanaishi kwenye dunia ya kisasa pamoja na kwenda na mabadiliko ya teknolojia kwenye upande wa kutuma na kupokea fedha kimtandao.

“Lengo letu kama kampuni siku zote imekuwa ni kutoa huduma na bidhaa ambazo ni za kipekee na ambazo zinapatikana kwa unafuu ili kuendana na maisha ya kila siku ya wateja wetu. Kwa kuzindua pokea fedha kutoka nchi Zaidi ya 200, tunaileta pamoja jamii kwa kuondoa mipaka kwani wote wataweza kupokea fedha moja kwa moja kwenye akaunti zao za Airtel Money kutoka mataifa mbalimbali,” amesema Nchunda.

Airtel Money ni moja ya huduma za fedha kwa njia ya simu za mkononi ambayo inakuwa kwa kasi huku ikiwa hapa nchini ikiwa imeunganisha na makampuni ya malipo ya huduma mbalimbali zaidi ya 1000, pamoja na kuunganisha na taasisi za fedha zaidi ya 40. Vile vile, Airtel Tanzania inazidi kupanua wigo kupitia Airtel Money Branch karibu yako ambapo kwa sasa ina maduka ya Airtel Money Branch zaidi ya 1200 ambayo yanatoa huduma na bidhaa zote za Airtel nchni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles