25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

VYUO VILIVYO NA IDADI KUBWA YA WANAFUNZI WA KIMATAIFA

1680Na FARAJA MASINDE

NJE ya vyuo 800 katika utafiti wa World University Rankings, hakauna hata chuo kimoja kutoka Marekani kilichochomoza kwenye 30 bora kwa kuwa na wanafunzi wa kimataifa.

Kwa mujibu wa utafiti wa Times Higher Education kwa vyuo vikuu duniani kwa mwaka 2015-16, hakuna chuo cha Marekani kilicho na zaidi ya asilimi 35 ya wanafunzi wa kimatifa ikilinganishwa na bara la Asia, Oceania na Ulaya.

Katika uchambuzi huo wa vyuo iimeonekana kuwa vyuo 16 kati ya 30 vyenye asilimia kubwa ya wanafunzi wa kimataifa viko Uingereza, huku saba vikiwa maeneo mbalimbali barani Ulaya na vinne vikiwa Australia au New Zealand.

Hii imekuwa na mshangao mkubwa kwa Marekani ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikionekana kuwa na vyuo bora zaidi duniani.

Katika kipindi cha mwaka 2013-14 Marekani ilikuwa na wanafunzi wa kimataifa zaidi ya 800,000 hata hivyo hali hiyo inaonekana kuwa tofauti kwasasa kutokana na wanafunzi wengi kwenda kwenye vyuo mbalimbali mbali na vile ya Marekani.

Hata hivyo licha ya kwamba marekani haijafua dafu kwenye 30 bora lakini bado imefanikiwa kupata uwakilishi kwenye orodha hiyo kupitia chuo American University of Sharjah kilichoko Umoja wa Falme za Kiarabu UAE ambacho kina asilimia 82 ya wanafunzi wa kimataifa.

Nyuma ya chuo hicho kuna chuo cha London School of Economics & Political Science cha Uingereza chenye asilimia 70 ya wanafunzi ambacho kinajumla ya wanafunzi kutoka mataifa 150 duniani.

Switzerland ni ya tatu kwa kuwa na wanafunzi wengi wa kimataifa hii imeelezwa kuchangiwa na vyuo vingi pamoja na gharama nafuu za masomo licha ya kwamba iko nje ya Umoja wa Ulaya.

Asilimia kubwa ya wanafunzi wa kimataifa kwenye vyuo 200 bora ni vya kimataifa na si vyuo vya binafsi kwani hakuna chuo cha binafsi kilichochomoza kwenye 30 bora.

Hata hivyo vyuo vya bara la Amerika licha ya kwamba havikuingia kwenye 30 bora lakini vimeweza pia kuwamo kwenye 200 bora kwa kuwa na wanafunzi wengi wa kimataifa.

Vyuo hivyo ni Carnegie Mellon University kilichoko mji wa Pittsburgh, Pennsylvania kilichoshika nafasi ya 37 kikiwa na wanafunzi wa kimataifa ambao ni chini ya asilimia 35.

Kingine ni Imperial College London, ambacho kimejielekeza kwenye sayansi na uhandisi ambacho kimenyakua nafasi ya 30 kwa kuwa na wanafunzi wengi wa kimataifa kwa asilimia 16 huku kikishika nafasi ya 18 duniani.

Chini ni orodha ya vyuo vilivyochanua kwenye utafiti huo na wastani wa wanafunzi kwenye mabano pamoja na nchi husika.

American University of Sharjah cha UAE (80), London School of Economics and Political Science (69.7) cha Uingereza,  Royal College of Surgeons in Ireland (62.5), École Polytechnique Fédérale de Lausanne (54.4) cha Switzerland na University of Luxembourg (51.7) cha Luxembourg.

Vingine ni Imperial College London (50.7), City University London (50.1) vyote vya Uingereza, Maastricht University (47.7) Uholanzi, University of St Andrews (46.9),a

University College London (45.9) vyote vya Uingereza na Macquarie University (44.1) cha Australia.

Vingine ni Middlesex University (43.7), University of Westminster (43.4) vyote vya Uingereza, Murdoch University (43.4) cha Australia, Heriot-Watt University (43.2), Uingere na Qatar University (42) cha Qatar.

Vingine ni Queen Mary University of London (40.2) cha Uingereza, University of Geneva (39.1) cha Uswizi, University of Essex (38.9) cha Uingereza na  University of Innsbruck (38.6) cha Australia.

Pia kuna vyuo kama Birkbeck, University of London (38.4) Uingereza,

Auckland University of Technology (38.2) New Zealand, Curtin University (37.9) Australia, University of Hong Kong (38) Hong Kong, University of Surrey(37.7), Brunel University London (37.5), King’s College London (37.2) vyote vya Uingereza, ETH Zurich–Swiss Federal Institute of Technology Zurich (37.1) cha Uswisi, Royal Holloway, University of London (36.7) na University of Warwick (36.6) cha Uingereza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles