29.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

VYUO VIKUU TANZANIA NI BORA-PROF. KUSILUKA

Makamu Mkuu wa Chuo cha Mzumbe, Profesa Lughano Kusiluka

Na JUSTIN DAMIAN-DAR ESA SALAAM

LICHA ya uwepo wa changamoto mbalimbali zinazoikabili vyuo vikuu hapa nchini, bado vyuo vingi vya ndani vina uwezo unaoridhisha wa kutoa elimu bora, inayooendana na mahitaji ya soko.

Makamu Mkuu wa Chuo cha Mzumbe, Profesa Lughano Kusiluka aliyasema hayo Dar es Salaam jana alipokuwa akizungumza na MTANZANIA,  baada ya kutembelea Kampuni ya New Habari (2006), Sinza Kijiweni.

Profesa Kusiluka alisema pamoja na changamoto hiyo hana shaka na elimu inayotolewa na vyuo vikuu vya ndani.

Alitaja baadhi ya changamoto hizo kuwa ni pamoja na ukosefu wa  madarasa ya kutosha, mabweni, kumbi za mihadhara, maabara na karakana kwa vyuo vinavyofundisha fani za sayansi.

“Pamoja na changamoto ya miundo mbinu inayoikabili vyuo vingi, bado wahitimu wake wanatoka wakiwa wameiva kutokana na msisitizo kutiliwa kwenye suala la ubora chini ya usimamizi wa Tume ya Vyuo Vikuu (TCU).

“Vyuo vyetu vingi vinatoa taaluma nzuri, Tanzania ni nchi ambayo uchumi wake unaendeshwa na Watanzania na hata ukienda kwenye viwanda na maofisi mengi utakuta wanaofanya kazi ni Watanzania tofauti na nchi nyingine.

“Ukienda nchi kama Botswana, Lesotho, Swaziland, Namibia Afrika Kusini na nyinginezo utakuta Watanzania wengi wanafanya kazi katika sehemu mbali mbali.

“Hii ina maana kuwa elimu waliyoipata hapa nchini ni bora na ndiyo sababu ya kupata kazi hata nje ya nchi yao,” alisema.

Alisema changamoto zimekuwepo kwa kuwa Tanzania bado ni nchi maskini lakini alifafanua kuwa Serikali imekuwa ikifanya jitihada mbali mbali kuhakikisha kuwa elimu inayotolewa na vyuo vikuu inakuwa bora zaidi.

“Siku za hivi karubuni Serikali imetayarisha andiko la mahitaji ya miundo mbinu katika vyuo vikuu vya umma ambalo mimi nilikuwa naliratibu.

“Andiko hili linaonyesha nia ya dhati yakuboresha elimu inayotolewa na vyuo vikuu vya umma,” alisema Prof. Kusiluka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles