29.9 C
Dar es Salaam
Friday, May 24, 2024

Contact us: [email protected]

Vyo Vikuu vya Mzumbe, California – Berkeley vyaanzisha uhusiano

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Chuo Kikuu cha California – Berkeley, Marekani, kimeanzisha uhusiano na ushirikiano na  chuo kikuu cha Mzumbe lengo likiwa ni kuimarisha na kukuza taaluma katika maeneo bobevu hususan maendeleo ya sayansi ya mazingira, utawala, sera na usimamizi.  

Prof. Youjin B. Chung, kutoka Chuo Kikuu Cha California –Berkeley, akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Chuo Kikuu Mzumbe, Kampasi Kuu Morogoro.

Akizungumza wakati wa kikao na Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. William Mwegoha, Prof. Youjin B. Chung, Mtaalamu wa maendeleo ya sayansi ya mazingira, sera na usimamizi kutoka Chuo hicho amesema wamevutiwa na maeneo ya ubobevu na tafiti yanayotolewa na Chuo Kikuu Mzumbe na hivyo kuanzisha ushirikiano huo ni muhimu na bora baina ya vyuo hivyo kwani utasaidia kukuza maeneo ya utafiti na taaluma.

Akizungumza katika kikao hicho, Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. William Mwegoha, amesema Mzumbe ni sehemu sahihi na bora ya kuanzisha, kukuza na kuendeleza ushirikiano katika maeneo ya ubobevu wa kitaaluma na tafiti na kwamba Chuo Kikuu Mzumbe kiko tayari kutoa ushirikiano katika kuhakikisha malengo ya ushirikiano baina ya vyuo hivyo yanafikiwa. 

Akielezea hatua za ushirikiano huo, Kaimu Mkurugenzi wa Mahusiano ya Kimataifa na Baraza la Wahitimu, Dk. Lucy massoi , amesema wamejizatiti kuhakikisha ushirikiano na taasisi za kimataifa zinazohusu tafiti na masuala ya elimu ya juu unaanzishwa na kuendelezwa, na kwamba tayari wameandaa mkataba wa mashirikiano na chuo cha Berkeley ambao unaonyesha maeneo ya ushirikiano, na utasainiwa wakati wowote ukisharidhiwa na pande zote. 

Kikao cha Utambulisho na maridhiano kilifanyika Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi Kuu Morogoro na kuhudhuriwa na baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ya Chuo hicho.

Prof. Youjin B. Chung, kutoka Chuo Kikuu Cha California, Berkeley (Katikati) akiwa na viongozi wa Menejimenti wa Chuo Kikuu Mzumbe.
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles