25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Vurugu zaiweka njia panda Yanga

Jamal Malinzi
Jamal Malinzi

NA ADAM MKWEPU, DAR ES SALAAM

MABINGWA wa soka Tanzania Bara, Yanga huenda ikakumbana na rungu la Shirikisho la Soka Afrika (CAF), baada ya vurugu kujitokeza katika mchezo wao wa Kombe la Shirikisho dhidi ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) uliochezwa Jumanne wiki hii katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi, alisema anaiombea Mungu Yanga ili isikumbane na adhabu ya CAF kutokana na matukio ya vurugu yaliyojitokeza katika mchezo huo wa Kundi A.

Alisema vitendo vilivyojitokeza vilishuhudiwa na kamisaa wa mchezo huo hivyo vinaweza kuiathiri Yanga na kujikuta ikipewa adhabu kali ya CAF iwapo kamisaa ataorodhesha kwenye ripoti yake.

Malinzi alisema Yanga waliruhusiwa kutumia Uwanja wa Taifa kwa ajili ya mchezo dhidi ya TP Mazembe kwa masharti ya kulinda miundombinu na usalama wa watazamaji.

“TFF tunafuatilia kwa karibu ili kujua uamuzi utakaotolewa na CAF kutokana na ripoti za msimamizi na kamisaa wa mchezo kuhusu matukio yaliyotokea nje ya uwanja kabla na wakati wa mechi,” alisema.

Katika hatua nyingine, TFF inatarajia kumfikishaa Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro, katika kikao cha Kamati ya Maadili ya shirikisho hilo kutokana na vitendo vyake vya kupinga maamuzi ya shirikisho hilo na kulishambulia kwenye vyombo vya habari.

Barua iliyotumwa kwa Muro ikiwa na sahihi ya Katibu Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa, imemtaka msemaji huyo kufika kwenye kamati hiyo ambayo itakutana kesho saa 4:30 asubuhi katika ofisi za shirikisho hilo.

Kabla ya mchezo wa Yanga na TP Mazembe, Muro alinukuliwa mara kwa mara kwenye vyombo vya habari akipingana na maamuzi ya TFF, ambapo juzi usiku alisambaza taarifa katika mitandao ya kijamii akidai TFF imepania kumfungia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles