30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

VITA YA UMEYA KIGAMBONI YAPAMBA MOTO

*Mmoja wa watuhumiwa ajitosa, CCM kuamua


 

b1

– dar es salaam

VITA ya kuwania umeya wa Manispaa mpya ya Kigamboni, Dar es Salaam, imepamba moto huku baadhi ya madiwani wakilazimika kutoa tamko la kukionya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Hatua hiyo imekuja baada ya baadhi ya madiwani waliojitosa kutaka nafasi hiyo, kudaiwa kutokuwa na sifa, hali ambayo inaweza kuhatarisha uhai wa CCM wilayani humo.

Akizungumza na MTANZANIA juzi, mmoja wa madiwani wa Viti Maalumu wa CCM ambaye hakupenda kutajwa jina lake, alisema hatua ya baadhi ya wagombea wanaohusishwa na makandokando ikiwamo tuhuma za wizi, nao kujitokeza kutaka kuwania nafasi hiyo, inaweza kukiua chama hicho tawala.

Hadi sasa majina ya madiwani waliojitosa kutaka kuwania nafasi hiyo kwa upande wa CCM ni pamoja na aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Temeke kwa kipindi cha mwaka 2010/15, Maabadi Hoja, Hemed Zahoro na Dotto Msawa.

Diwani huyo wa viti maalumu, alisema uwepo wa mmoja wa madiwani kwenye kinyang’anyiro hicho si sawa kutokana na rekodi yake ya matukio kwa jamii kuwa si nzuri.

“Sisi ndiyo tutaenda kupiga kura kule ndani, hofu yetu ni kama tutapitishiwa mtu ambaye hana historia ya kueleweka katika uadilifu, itatulazimu kufanya uamuzi mgumu kwa ajili ya Kigamboni na si chama

“Huyu diwani alisharipotiwa katika vyombo vya habari kuwa alishafikishwa mahakamani kwa tuhuma za wizi wa gari mkoani Morogoro, na wakubwa na wenye fedha ndiyo wanambeba kwa ardhi ya Kigamboni, hii itachafua taswira ya wilaya yetu na chama kwa ujumla,” alisema diwani huyo.

MTANZANIA ilipomtafuta Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Temeke, Yahya Sikunjema ili kupata ufafanuzi wa suala hilo, simu yake iliita bila kupokewa.

Alipotafutwa Msemaji wa CCM, Christopher ole Sendeka, alisema Kamati Kuu ya Taifa inatarajia kukutana hivi karibuni kujadili kwa kina majina ya wagombea na yule mwenye sifa atapitishwa kuwania nafasi hiyo.

Kigamboni ni wilaya pekee iliyosalia kufanya uchaguzi wa meya, baada ya Ubungo kufanya hivi karibuni jambo ambalo linakwamisha shughuli za maendeleo.

Hivi karibuni iliripotiwa kutiwa mbaroni kwa Diwani Msawa kwa tuhuma za wizi wa gari na kufunguliwa kesi namba 633 mkoani Morogoro.

Katika kesi hiyo, alihusishwa na Chrisopher Nyakiaga ambao wote walituhumiwa kujihusisha na wizi wa gari aina ya Toyota Coaster lenye namba za usajili T 615 BUL mali ya George Kavishe, mkazi wa Kihonda mkoani mkoani Morogoro

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles