28.2 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Virusi vya corona vyakosesha watu burudani msimu wa Pasaka

Mwandishi Wetu

TUNAWEZA tusisahau kuhusu mlipuko wa vya corona vinavyosababisha watu wazuiwe kutoka nje. Lakini mwishowe bado tutaendelea kuzungumza pamoja.

Kwa sababu ukiachilia mbali wasiwasi wetu kuhusu virusi vya corona, inaonekana kutakuwa na hofu kwa baadhi ya familia kuishi juu ya wengine nyumbani kwao.

Mtafiti wa Masuala ya Uhusiano kutoka Chuo Kikuu cha Open, Profesa Jacqui Gabb, anasema katika hali ya kawaida, wapenzi au wanandoa huwa wanakaa pamoja kwa muda wa nusu siku, lakini hiyo ilikuwa kabla ya virusi vya corona, lakini sasa hali ni tofauti na wapenzi inabidi wakae zaidi ya saa 15 au 16 wakifanya kazi pamoja huku watoto nao wakisomea nyumbani.

Hali hii inafanya watu kuwa karibu zaidi tofauti na ilivyokuwa nyuma.

“Hatujawahi kupitia kipindi kama hiki,” anasema Profesa Gabb.

Familia kuwa pamoja kwa muda mrefu na kufanya shughuli zote pamoja huwa ni wakati wa sikukuu za Krismasi, kipindi ambacho watu wako likizo.

Lakini sasa marufuku ya kutotembea nje ili kujikinga na maambukizi ya corona yamebadilisha mfumo wa maisha.

Familia wakiwa pamoja wakati wa sikukuu ya Krismasi huwa wanapika pamoja na kufurahi pamoja, lakini sasa familia ziko pamoja zikiwa na hofu, msongo wa mawazo na huzuni kwa pamoja.

Wengine wakiwa wana hofu ya ajira zao, fedha walizonazo hazitoshi kujikimu, uangalizi wa watoto, kuwa huru kufanya vitu unavyoweza kufurahia na marafiki na wasiwasi mwingi tu.

Wazazi

“Mimi nnamlea mwanangu peke yangu, kipato changu tu ndio tunakitegemea. Ninaweza kufanya kazi nyumbani lakini naona kuwa ni jambo ambalo haliwezekani nikiwa na watoto wangu wa miaka sita na kumi.

Ninaweza kupoteza muda mwingi na kipato nisichotaka kukipoteza.

Mtoto wangu haendi shule na tunaishi na mama yangu mwenye miaka 84. Yaani ninajiona kuwa sina namna nyingine.

“Hakuna uhuru wa kufanya mambo yako,” anasema mwanasaikolojia Dk. Caroline Schuste.

Wakati huu unafanya watu wakose muda wao binafsi, wanakuwa hawana raha hata kama wapo na familia zao.

Anaongeza: “Ukiwa na watoto, maisha ambayo mtu umezoea kuishi yanakuwa hayapo tena.”

Msichana

”Wazazi wangu wanaudhi. Nikishuka ngazi na kusema ‘asubuhi njema’ na wao watasema ‘mchana mwema’. Ni kama vile sawa mimi ni mvivu, naelewa.

Habari ya kutotoka nje imekuwa ikionekana kupitia kwenye macho ya walionacho na si wasionacho, anaeleza Profesa Gabb. ”Si rahisi kama ilivyo rahisi kuweka video ya mazoezi na kujenga uhusiano na kila mtu,” anaeleza.

Naungwa mkono na utafiti wa Save the Children, shirika hilo likiwahofia wazazi wakati wa amri ya kutotoka nje kama wanapata chakula cha kutosha, kama wanawasaidia watoto kazi za shuleni, pia kuhusu fedha.

Watoto wanahofu mtu mmoja wa familia yao akiugua, kupungua kwa chakula na kutoonana na marafiki

Mwalimu mmoja kutoka Hastings alituma ujumbe akuwaambia wazazi ”kutojiumiza au kujihisi wakosaji” wakati wa siku hizi za kukaa ndani.

”Usijifanye kuwa shujaa,” anawaambia.

Tunapojisikia kuwa hatuwezi kudhibiti hali ya msongo wa mawazo na kusema kuna namna nyingi za kushughulika na hali hiyo.

Mara tu watu wanaweza kuonesha kupenda kufanya mazoezi au kufanya usafi wa nyumba zao au bustani, kuwapa mtazamo kuwa wana ile nguvu ya kudhibiti vitu.

Mkuu wa shule

“Hakika haiwezekani kusimamia usomaji kwa njia ya mtandao kwa mwanafunzi wa shule ya msingi na kufanya kazi kutokea nyumbani wakati huo huo. Wazo hilo halina maana acha sasa.

Kuna shughuli nyingine ambazo mtoto wako atajifunza lakini suala la kutilia maanani hapo ni kazi yako. Acha kuonesha wewe ni shujaa.”

Lakini Dk. Shah anasema: “Tusijiwekee wazo kuwa suala hili litakuwa gumu kwetu.”

Dk. Shah anasema bado tu natafuta kitu gani kinaweza kuwa msaada wa kufanya tujisikie vizuri kipindi hiki.

Inaweza kuwa suala la hofu na mavazi kutokana na hali ya kutotoka nje.

Kwa sababu kwa suala lake, Dk. Shah anasema hujisikia vizuri zaidi anapokuwa amevalia mavazi nadhifu ya kazini anapofanya kazi kutoka nyumbani, hata kama huwashangaza watu wanapokuwa kwenye mkutano kwa njia ya simu (video conference).

Lakini kuna maneno ya kutia moyo kwa kila mmoja ambaye anapata wakati mgumu kufanya kazi kwenye kompyuta au mikutano ya simu za video.

Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi alituma ujumbe akiwaambia wazazi “kutojihisi kuwa wakosaji” katika majuma haya yenye kukanganya.

“Acheni kujaribu kuwa mabingwa,” anasema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles