25.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Viongozi wa dini wamuomba Rais Samia kuendeleza mema ya Magufuli

Na Sheila Katikula, Mwanza

Viongozi wa dini na watumishi kutoka Sekta mbalimbali wa jijini hapa wamemuomba Rais Samia Suluhu Hassan  kuendeleza mikakati iliyokuwa ikifanywa na aliyekuwa Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dk. John  aliyefariki Machi 17, mwaka huu.

Hayo yamebainishwa na viongozi hao kwa nyakati tofauti wakati wakizungumza na waandishi wa habari jijini hapa  kuhusu  kifo cha aliyekuwa   wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hayati Rais John Magufuli.

Aidha, Katibu wa Chama  cha Walimu Wilaya ya Maswa (CWT) Froling Rwela, amesema ni vema Rais Samia Hassan Suluhu kufuata nyayo zilizoachwa  na hayati Mafuguli kwa kukamilisha miradi ambayo haijakamilika ili wananchi waweze kupata huduma stahiki.

Amesema lengo la hayati Dk Magufuli lilikuwa ni  kuleta maendeleo kwa wananchi ndiyo maana alikusanya kodi na kuhakikisha kila senti inaingia Serikalini nakuanzisha miradi mbalimbali nchini.

Hata hivyo amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kushika nafasi hiyo kama katiba inavyosema sanjari na kumuomba kudhibiti nidhamu ya watumishi wa umma kwani ni watu muhimu katika kuendeleza nchi lakini wakiachwa huru watafanya wanayotaka wao na kutowajali wananchi pindi wanapihitaji msaada.

“Ninamuomba Rais Samia kuendelea kudhibiti nidhamu kwa watumishi wa ummakwani wao ni muhimu sana katika jamii lakini wasipofatiliwa kwa karibu na kudhibitiwa watafanya wanachotaka wao kwa sababu ni binadamu kitendo ambacho siyo kizuri na hatutaweza kifikia malengo ya hayati Magufuli na vile sisi walimu tunamiaka mingi hatujaongezewa mshahara tunaomba Mama Samia atufukilie,” amesema Rwela.

Kwa upande wake, Katibu wa Kanisa la EAG Tanzania, Mchungaji Robert Ngai, amesema kifo cha aliyekuwa Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Magufuli kimewashtua watu wengi kwa sababu ya kutopata taarifa za kuugua kwake lakini kwa sababu  ni kazi ya Mungu haiwezi kuwasahihi kwani kila nafsi itaonja mauti.

“Tumemupoteza Rais Magufuli amezima kama mshumaa katika ya giza nene lakini ghafla mshumaa umewashwa na umemlika  na kulet a mwanga tunaimani na aliyevaa kiatu cha Magufuli atafuata nyayo zake kwa vitendo kwani yeye siyo Mwanamke wa kwanza kuwa kiongozi, hata katika biblia kuna mwanamke aitwaye Debora aliongoza wanaumwe Elfu kumi alitangulia mbele na ushindi ulipatikana  kwani kupitia hili tunaimani na Rais Samia Suluhu Hassan,” amesema Mchungaji Ngai.

Aidha  Mkuu wa  Chuo cha Mwanza Christian College, Dk. Agrey Mwakisole, amesema Rais Magufuli alifanya mambo mengi lakini alimgusa kutokana na moyo wake wa utekelezaji wa kufanya aliyoyaamini hakuteteleka kuyatekeleza ikiwamo kupeleka umeme, Maji Vijijini, kujenga vituo vya afya kila sehemu kufanya ukarabati kwenye shule zote kongwe nchini, watoto kusoma bure kwanzia kidato cha kwanza hadi cha nne  kutokana na utendaji huo wa kazi hawezi kusahaulika mioyoni mwa watu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles