30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Vijana, wasomi watakiwa kuchangamkia jukwa la Mchongoo kujikwamua kimaisha

Na Daines Msumeno (TUDARCo), Mtanzania Digital

KATIKA kupambana na tatizo la ajira na umasikini nchini, watu wenye ujuzi mbalimbali, talanta na elimu wamepewa namna ya kupata fursa katika jukwaa jipya la Mchongoo ambalo litawaunganisha na Wizara, Taasisi na Sekta binafsi katika kujiinua kiuchumi.

Aidha, katika kufanikisha hilo watu hao wataunganishwa na watoa huduma na wanaotafuta huduma na kujumuisha biashara zote, mashirika, na vyama katika ngazi za kitaifa, kikanda, na bara.

Hayo yamebainishwa leo Alhamisi Oktoba 7, 2021 na Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Jukwaa hilo, Julius Wambogo, ambapo amesema wanatumia teknolojia ya digitali ikiwa ni njia mpya ya kupata na kutoa huduma zinazosaidia kufanya kazi katika maisha ya kila siku.

Kila mwaka kampuni wanafanya mambo tofauti ili kuongeza mauzo na shughuli zao, kusaka wajuzi na wataalam ila wanatumia nguvu nyingi na mitandao mingi sababu hakuna sehemu moja wanayopatikana na mara kwa mara wanatakiwa.

Amesema Mchongoo ni jukwaa linalowaunganisha watoa huduma mbalimbali hatua itakayotoa fursa mbalimbali.

“Mchongoo.com inakusudia kukusanya watoa huduma kuboresha utafutaji huo ili kutoa mahali ambapo kuna wenyeubunifu, wenye talanta na wenye uzoefu ambao wanaweza kuonyesha ujuzi wao na ili waweze kupatikana kwa urahisi.

“Pamoja nakuwa wazi kwa sasa tunapanga kuzindua rasmi mapema mwakani 2022, na itawagusa watu binafsi, makampuni, miradi ya shirika na ya viwandani, kwenye mtandao wa watoa huduma wenye ujuzi, wabunifu ambao wana utaalamu katika sekta mbalimbali katika nyanja za kazi ili kuungana na kufanya kazi kwa urahisi,”amesema Wambogo.

Aidha, Wambogo amefafanua zaidi kuwa dhumuni jingine ni kubadilisha soko la kazi na utoaji wa huduma na kujenga tena kile kilichoathiriwa na changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na Uviko-19.
“Mchongoo tunahitaji msaada wako na ushirika wako wasiliana nasi ili kujitolea au kuwekeza asannte, hivyo kupitia teknolojia tumekusudia kubadilisha soko la ajira na utoaji huduma kwa kuboresha namana ya uapatikanaji, hii ni kutokana na athari mbalimbali zilizochangia kuyumba kwauchumi ikiwemo ugonjwa wa Corona,”amesema Wambogo.

Ameongeza kuwa katika Mchongoo ni huduma aina zote hutolewa kupitia jukwaa hilo la mtandaoni kwa kushirikiana na sekta binafsi, wizara na mataifa yenye dhumuni la kukuza uchumi wao na kuimarisha ubunifu pamoja na kuondoa umasikini katika jamii na kwamba mtandao huo ni muongozo.

Kuhusu changamoto ya ajira kwa vijana wanaohitimu vyuo, Wambogo amesema kila mwaka zahidi ya wahitimu 1,000 humaliza masomo yao huku wengine zaidi ya 1,000 pia wakishindwa kuendelea na masomo kutokana na ukosefu wa fedha.

“Pamoja na kwamba wanafunzi hao wanashindwa kuendelea na masomo makampuni mengi huingia sokoni kutafuta wataalamu mbalimbali kila mwaka baadhi ya makampuni bila mafanikio yakupata wanacho tafuta na kusahili,

“Utafutaji huu huchukua muda na nguvu ya watendaji wa makampuni kwani uhitaji wa wataalamu unakuwa mkubwa,”amesema Wambogo.

Wambogo amehimiza kuwa jukwaa la https://mchongoo.com itakuwa ni sehemu ya kutatua changamoto mbalimali za ajira kwa vijana na utafutaji ya watoa huduma wabunifu, wenye ujuzi na elimu wataonyesha ujuzi wao na kupatikana kwa urahisi kwaunganisha na watafuta huduma binafisi na makampuni yenye uhitaji,

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles