28.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 18, 2024

Contact us: [email protected]

VIJANA WANAOTUMIA DAWA ZA KULEVYA WAPATIWA MSAADA

Na RAMADHAN HASSAN-DODOMA


dawa-za-kulevyaVIJANA wanaojihusisha na matumizi ya dawa za kulevya mjini hapa, wamepatiwa msaada wa vyakula na Jumuiya ya Ahmadiyya Jamaat Tanzania, Kanda ya Kati.

Akizungumza na vijana hao 15 katika kituo cha Pedderef Sober House kilichopo Dodoma Makulu, baada ya kuwakabidhi msaada huo, Sheikh wa kumuiya hiyo Kanda ya Kati, Basharat Butt, aliitaja misaada hiyo ni pamoja na unga, mchele, sukari na maharage vyenye thamani ya zaidi ya Sh 300,000.

Alisema msaada huo ametoa kwa vijana hao kuwawezesha kushiriki kwa pamoja katika kipindi hiki cha mwaka mpya.

“Jumuiya yetu imefurahishwa na kitendo cha vijana hawa kuonyesha dhamira yao ya kuachana na matumizi ya dawa za kulevya, ndiyo maana tumependa kushiriki kwa pamoja nao mwaka huu kwa kuwapatia zawadi.

“Ni wakati sasa kwa jumuiya na taasisi nyingine kuwaunga mkono vijana hawa ambao wameamua kukaa kwa pamoja na kujitegemea kwa kufanya kazi mbalimbali zinazowaingizia kipato wakiwa kituoni hapa,” alisema.
Aidha, aliwataka vijana hao kuwa mabalozi wazuri kwa wenzao ambao bado wapo maeneo mbalimbali wakitumia dawa hizo.

Kwa upande wake, Kaimu Meneja wa kituo hicho, Adam Lupatu, aliomba jumuiya na taasisi nyingine kuwasaidia kwa kuwapatia vitendea kazi vya kiufundi ili waweze kujiinua kiuchumi zaidi.
“Ni matumaini yetu vijana wengine watajiunga ili waweze pia kushiriki katika shughuli za kimaendeleo,’’ alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles