Salome Bruno,TUDARCo
Katika ulimwengu wa sasa kumekuwa na wimbi kubwa la vijana kukosa ajira sio kwa wasomi hata kwa wasiosoma. Janga hili limekuwa ni kubwa kwa kushindwa kutambua fursa zilizopo katika mazingira yanayotuzunguka kwa ujumla wake.
Vijana wengi hawana uthubutu wa kuweza kutambua fursa katika mazingira yao husika, wengi wao wamekuwa wakiilaumu serikali kwa kukosa ajira kutokana na mazingira yaliowakuza hayawajengi kutafuta na kutambua fursa zilizopo kwenye jamii yetu.
Hii yote inatokana na mfumo wa serikali yetu katika elimu ambayo inasimamia. Kwani inatujenga kuwa watu wa kuajiriwa na sio kujiari sisi wenyewe ……Daah inasikitisha sana ivi ni nani alaumiwe kati ya mitaala yetu au sisi vijana ?
Jibu linakuja hakuna wa kulaumiwa zaidi ni kutambua fursa zilizotuzunguka pamoja na kujifunza kwa waliofanikiwa katika nyanja mbalimbali za kijamii.
Kumekuwa na wasomi wengi walioweza kufanikiwa kufika mbali kwa kutambua fursa zinazowazunguka na kuzifanyia kazi kwa jamii na kuleta manufaa katika jamii zao.
Hivyo basi ni jukumu la kila kijana kutambua fursa mbalimbali zinazotuzunguka katika jamii ili kuondokana na janga la ajira lililopo katika jamii.