22.8 C
Dar es Salaam
Thursday, October 6, 2022

KMC yanogewa na Dante

Na Winfrida Mtoi

UONGOZI wa Klabu ya KMC umempa mkataba mpya wa mwaka mmoja beki wake Andrew Vincent ‘Dante’, kuendelea¬† kutumikia kikosi hicho katika msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2021/2022.

Dante alijiunga na KMC msimu uliopita akitokea Yanga na ameonesha kiwango kizuri akijihakikishia namba  katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo.

Mchezaji mwingine aliyeongezewa mkataba na KMC ni kiungo  Jean Baptiste Mungiraneza, raia wa Rwanda.

Katika kuboresha kikosi chake, timu hiyo ya Manspaa ya Kinondoni, imekamilisha usajili wa wachezaji kadhaa  waliotamba msimu uliopita akiwamo kipa Farouk Shikalo aliyekuwa Yanga, Hassan Kessy akitokea Mtibwa Sugar na Mohammed Kassim kutoka Polisi Tanzania.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,814FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles