27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Vijana 2000 wakutanishwa kuunda timu 32 za mpira wa miguu, pete

ELIYA MBONEA – ARUSHA

VIJANA zaidi ya 2000 wanaoishi katika mazingira magumu kutoka mikoa 13 ambao wanalelewa na Shirika la Kimataifa la Compassion Tanzania (CIT), wamekutanishwa mjini Arusha ili kuonyesha vipaji vyao katika mchezo wa mpira wa miguu na mpira wa pete.


Lengo kuu la kuwakutanisha vijana hao ni kuibua vipaji miongoni mwao na baada ya michezo hiyo watachujwa hadi vijana 550 watakaunda timu 32, ambapo timu 16 zitakuwa za mpira wa miguu na 16 zitakuwa za mpira wa pete.

Mkurugenzi wa shirika hilo, Agnes Hotay amesema mashindano hayo yaliyoanza Desemba 17 yatakamilika Desemba 21 mwaka huu.

“Tumewakutanisha pamoja kwanza kuibua, kukuza vipaji vya michezo lakini pia kuboresha afya zao kama vijana tukiwa na lengo la kuhamasisha kwa uanzishaji wa shule za vipaji kwenye kanda hii ilivipaji hivyo viweze kupata sehemu ya kuendelezwa,” amesema Agnes.

Baadhi ya vijana watakaoshindanishwa kwenye michezo hiyo wamepongeza shirika hilo kuwakutanisha huku wakidai mashindano hayo yatawasaidia kufahamiana zaidi na vijana wenzao na pia yatasaidia kuonyesha vipaji vyao na baadae kuwa ajira zao za baadae.

Shirika hilo kwa ushirikiano wa Makanisa ya Kiinjili uhudumia watoto na vijana wahitaji kwa lengo la kuwawezesha kutoka katika utegemezi na kuwa na maisha binafsi ya kujitegemea.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles