32.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

VIGOGO BOT KUHOJIWA LEO

Na ELIZABETH  HOMBO – DODOMA


SIKU chache baada ya Spika wa Bunge, Job Ndugai kuagiza Kamati ya Hesabu za Serikali na Mashirika ya Umma (PAC), kukutana na bodi ya menejimenti ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT),  Mwenyekiti wa PAC, Naghenjwa Kaboyoka amesema tayari wamewaita kwa ajili ya mahojiano.

Jumanne wiki hii, akichangia bajeti ya Wizara ya Fedha, Mbunge wa Ulanga, Gudluck Mlinga (CCM), alisema    fedha za matibabu ya maofisa wa BoT kwa mwezi ni Sh bilioni 12, lakini wangekuwa wanatumia mfuko wa NHIF matibabu yao kwa mwezi yangekuwa Sh bilioni moja tu.

“Hivi ninavyoongea watumishi wa BoT ndiyo taasisi inayotumia fedha nyingi katika matibabu bila msingi wowote.

“Mfanyakazi akiwa na mafua anakwenda kutibiwa India wanatumia fedha nyingi na wamesahau kuwa fedha hizi ni za walipa kodi,” alisema Mlinga.

Kwa sababu hiyo Spika Ndugai alisema: “PAC muite bodi ya BoT na uongozi wa juu kabla ya kukaa na BoT muwe mmekaa na Mlinga kuhusu jambo hili.

“Halafu mkae na NHIF (Mfuko wa Bima ya Afya), halafu mnaita BoT baada ya hapo mniletee haraka   majibu ya kazi yenu   niweze kumwandikia Rais  aingilie kati,”alisema Spika Ndugai.

Akizungumza   na MTANZANIA jana, Kaboyoka ambaye pia ni Mbunge wa Same Mashariki (Chadema) alisema tayari   bodi ya BoT imeitwa  na kuhojiwa kuhusiana na tuhuma hizo.

“Kama alivyoagiza Spika wa Bunge, tayari tumewaita na tutakutana nao leo (jana) na baada ya hapo tutawasilisha taarifa kwa Spika,”alisema.

Juzi kamati hiyo ya PAC ilimhoji Mbunge huyo wa Ulanga kuhusiana na tuhuma   alizozitoa dhidi ya BoT.

BoT inatuhumiwa kutumia bima binafsi badala  ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles