24.2 C
Dar es Salaam
Monday, September 26, 2022

ONGEZEKO LA TAKA ZA PLASTIKI KUPUNGUZA SAMAKI BAHARINI

Veronica Romwald, Dar es Salaam            |


Wakati dunia inaadhimisha Siku ya Bahari leo, Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Masuala ya Mazingira (UN Environment) linakadiria kuwa ifikapo 2050 samaki baharini watapungua kwa kiasi kikubwa.

Shirika hilo linaeleza hali hiyo ni kutokana na ongezeko la taka za plastiki baharini linalofanya uwiano wa idadi ya samaki kuwa mdogo kuliko taka hizo.

Hayo yameelezwa Dar es Salaam leo Ijumaa Juni 8, na Ofisa Mwakilishi wa UN Environment Tanzania, Clara Makenya alipozungumza na Mtanzania Digital ofisini kwake.

“Inakadiriwa kila mwaka takribani mifuko ya plastiki trilioni tano zinazalishwa ulimwenguni kati ya hizo, tani milioni 13 zinaishia baharini hatua ambayo kwa kiwango kikubwa inaathiri samaki pamoja na viumbe hai vingine.

“Utashi wa kisiasa unahitajika kwa kiasi kikubwa katika kutengeneza sheria, kutunga sera na kuzisimamia ili kupambana na ongezeko la taka za plastiki baharini,” amesema.

Aidha, Makenya amesema suala hilo lisipotazamwa kwa ukaribu na haraka huenda dunia ikatangaza kuwa ni janga jingine dhidi ya uharibifu wa mazingira na viumbe hai baharini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,044FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles