23.3 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

‘Vifo vya mama wajawazito, watoto vikomeshwe’

PregnantWomanNa Mwandishi Wetu, Mbeya

JAMII imetakiwa kuhakikisha vifo vitokanavyo na matatizo ya uzazi kwa akina mama wajawazito na watoto nchini vinatokomezwa
Hayo yamesemwa jana na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Mpoki Ulisubisya, alipotembelea zahanati ya Kijiji cha Uturo kilichopo wilayani Mbarali ambacho wananchi wa kijiji hicho wanashiriki katika kuondoa matatizo hayo.
Dk. Mpoki alisema Serikali katika kutekeleza sera ya afya nchini, inahakikisha akina mama wajawazito na watoto wachanga hawafi kwa magonjwa yanayozuilika
“Gharama za afya zimekuwa kubwa sana, hivyo nguvu yetu na umoja ndiyo njia pekee ya kujikomboa na kuleta maendeleo ya nchi na kutokomeza vifo vya akina mama nchi nzima,” alisema.
Kutokana na hali hiyo, aliwataka wananchi kujua afya ni wajibu wa kila mtu na inawezekana endapo kila mtu atajitolea kuhakikisha huduma za afya zikiwemo za kliniki badala ya kuendelea na utamaduni wa kujifungulia nyumbani.
Hata hivyo, Katibu Mkuu huyo, aliitaka mikoa mingine kwenda katika kijiji hicho kwa ajili ya kujifunza namna gani wamefanikiwa kuwashirikisha wananchi wote hususani akina baba kushiriki kuanzia ujauzito hadi mtoto anapozaliwa.
Kwa upande wake Mganga wa Zahanati hiyo, Wilson Chotamganga, alisema kijiji hicho kimefanikiwa kutokomeza vifo hivyo kwa kuunda timu ya viongozi wa vitongoji wa huduma za uzazi na mtoto pamoja na kuanzisha madaftari mawili ya mama wajawazito na watoto chini ya miaka mitano.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles