27.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

VIFAA VYA SHULE SASA DILI KWA MACHINGA

Na TUNU NASSOR-DAR ES SALAAM


 

vifaa-vya-shuleBAADHI ya wafanyabiashara ndogondogo maarufu machinga wa Jiji la Dar es Salaam, wamechangamkia fursa ya kuuza vifaa vya shule katika mitaa mbalimbali ya jiji hilo ikiwa ni siku chache kabla ya kufunguliwa shule.

MTANZANIA jana lilishuhudia mitaa mingi ya Kariakoo na Manzese ikiwa na machinga wakiuza bidhaa za shule zikiwamo masanduku ya chuma, mabegi ya shule, sare za shule, vitabu, daftari na kalamu.

Katika uchunguzi huo, machinga hao wamekuwa wakiuza vifaa hivyo kwa bei sawa na ile ya dukani jambo ambalo linawarahisishia kupata wateja kwa urahisi.

Mmoja wa machinga hao, Hemedi Juma, alisema kuwa vifaa hivyo wanavipata katika maduka ya jumla ambapo wao huongeza faida kidogo.

“Bei tunayouza sisi ni sawa na wenye maduka ya jumla lakini watu kwa kuwa wamezoea kununua madukani ndio maana unaona msongamano ni mkubwa,” alisema Juma.

Katika duka maarufu la kuuza vifaa vya shule lililoko Kariakoo la Tahfif katika makutano ya mitaa ya Tandamti na Swahili, watu mbalimbali walikuwa wamepanga foleni ya kuingia dukani humo.

Maduka ya vitambaa vya sare za shule pia yalionekana yakiwa na watu wengi wakinunua bidhaa huku mafundi nao wakiendelea na kazi ya ushonaji.

Mmoja wa mafundi anayefanya shughuli zake katika eneo la Manzese Uzuri, Joachim Mkude, alisema kwa sasa nguo nyingi anazoshona ni sare za shule.

“Kwa sasa mafundi tumezidiwa na sare za shule kwa kuwa shule ziko karibu kufunguliwa na nguo zinahitajika haraka,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles