25.5 C
Dar es Salaam
Saturday, May 18, 2024

Contact us: [email protected]

Video za Ajib zatumwa Slovania

Ajib-mpiraNA SAADA SALIM

VIDEO za straika wa Simba, Ibrahim Ajib akiwa uwanjani akifanya mambo, zimegeuka dili baada ya Klabu ya FC Olimpija Ljubljana ya Slovenia na nchi nyingine kuzihitaji kwa ajili ya kutaka kuangalia uwezo wake.

Awali klabu hiyo ilimhitaji winga wa Azam FC, Farid Mussa, lakini ilishindikana mara baada ya uongozi wa timu hiyo kushindwa kufikia mwafaka na klabu hiyo ya Slovenia.

Akizungumza na MTANZANIA jijini jana, Meneja wa Mbwana Samatta, Jamal Kisongo ambaye mara nyingi anatumiwa na mawakala kutoka nje ya nchi, alisema baada ya dili la Farid kushindikana klabu hiyo imeagiza CD za Ajibu pamoja na Said Ndemla ili kuona uwezo wao.

Alisema tayari zoezi hilo limefanyika, kwani ameshatuma baadhi ya CD hizo kwa mawakala mbalimbali wa timu za nje, ikiwemo FC Olimpija ambayo inamhitaji kumsajili Ajib Juni mwaka huu.

“Unajua mara ya kwanza tulichelewa dirisha la usajili limefungwa, sasa hivi wameniambia nitume CD za mchezaji huyo pamoja na Ndemla kwa kuzingalia ili kufikisha katika benchi la ufundi ili wasajiliwe Juni mwaka huu kwenye usajili wa majira ya joto,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles