30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 30, 2023

Contact us: [email protected]

Kazi amshauri mwamuzi Simba, Yanga

Othman Kazi (12)NA ADAM MKWEPU, DAR ES SALAAM

ALIYEKUWA mwamuzi wa soka nchini, Othman Kazi amemshauri mwamuzi wa pambano la Simba na Yanga litakalochezwa Jumamosi hii, Jonesia Rukyaa, kutochezesha mchezo huo kwa mazoea badala yake azingatie sheria na mamlaka aliyonayo anapokuwa uwanjani ili kuwa kiongozi mzuri wa mchezo huo.

Kazi pamoja na waamuzi wenzake wasaidizi watatu Omary Miyala, Omari Mfaume na Kamwanga Tambwe mwaka 2009  walifungiwa kuchezesha soka maisha na Shirikisho la soka Tanzania (TFF), wakihusishwa na rushwa katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Mtibwa Sugar na Majimaji.

Akizungumza na MTANZANIA, Kazi alisema kuwa Jonesia anatakiwa kufahamu tabia za wachezaji na kuwa kiongozi wa mchezo huo na si kuwa chanzo cha vurugu ambazo zitachangia kupoteza ladha ya mchezo.

“Mwamuzi anatakiwa kuwa mwenye mamlaka yote ndani ya uwanja na kuwa kiongozi wa wachezaji bila ya kupendelea upande wowote,” alisema Kazi.

Kazi  alisema ameamua kutoa ushauri huo kutokana na baadhi ya wamuuzi kushindwa kuwaongoza  vema wachezaji, hivyo kuwa chanzo cha mchezo kuvurugika na kusababisha mashabiki na viongozi kulalamika.

“Tatizo la waamuzi wetu ni kushindwa kusoma mchezo pamoja na tabia ya wachezaji na kusababisha kutawaliwa katika mchezo.

“Namshauri dada yangu Jonensia kuwa makini siku hiyo, ajitahidi kuongozwa na sheria si kufuata rekodi zilizopita,” alisema Kazi.

Akizungumzia juu ya sheria inayotoa mamlaka ya mwamuzi kufungiwa maisha endapo atatoa taarifa ya rushwa, alisema kuwa TFF wameshindwa kutafsiri sheria hiyo.

“TFF wameshindwa kutafsiri sheria hiyo ambayo inamjumuisha mwamuzi anapotoa taarifa juu ya rushwa na kutakiwa kufungiwa maisha.

“Kinachotakiwa kufanyika ni kuchukuliwa ripoti kutoka kwa kamishna na mwamuzi wa mchezo huo, ili kufanya uamuzi na endapo mwamuzi akipata alama chini ya sita kwenye mchezo huo, atakuwa hafai na atastahili adhabu hiyo,” alisema Kazi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles