29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

Viboko vyapigwa marufuku shule za awali na msingi

Upendo Mosha, Moshi

Walimu wa shule za msingi wamepigwa marufu Kutoa adhabu ya viboko kwa wanafunzi wa shule za awali mpaka darasa la nne ili kuepuka athari zinazotokana na matumizi holela ya adhabu hizo nchini.

Sheria ya mtoto ya mwaka 2009 kifungu cha 13 pamoja na kanuni zake za mahakama za watoto zinapiga marufuku vitendo na matumizi ya adhabu zenye kudhalilisha na kuondoa utu wa mtoto ikiwemo viboko.

Naibu katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia na ufundi Dk. Ave-Maria Semakafu alisema hayo wakati anakagua mradi fursa kwa watoto unaotekekezwa katika mikoa ya Mwanza na Kilimanjaro.

”Kuna kesi zaidi ya nne zinaendelea katika mahakama mbalimbali nchi ambapo watoto wamepooza miili yao kutokana na adhabu holela za viboko zinazotolewa na walimu” alisema.

Aidha alisema sheria imetoa muongozo wa nani atoe adhabu kwa baadhi ya wanafunzi watukutu na kwamba wanaokwenda kinyume na sheria serikali haitawaacha.

Naye Mkurugenzi msaidizi wa elimu ya awali ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Dk. George Jidamva alitaka walimu kuepuka kukosea katika utoaji wa elimu ya awali hadi darasa la saba kwani huko ni kuangamiza kizazi kijacho.

”Hili suala la viboko liepukwe kwani linamuondolea mwanafunzi kujiamini, ubunifu, Kujituma na ujasiri walimu kuweni wabunifu katika kujenga nidhamu ya wanafunzi na siyo viboko” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles