Bashiru atuma salamu kwa wakuu wa mikoa Mwanza, Morogoro

0
1270

Derick Milton, Simiyu

Katibu Mkuu wa Chama cha mapinduzi (CCM), Dk. Bashiru Ally, amewataka wakuu wa mikoa ya Mwanza na Morogoro kutekeleza wajibu wao ipasavyo na siyo kumsubiri Rais aje kutekeleza katika maeneo yao.

Dk. Bashiru ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Agosti 8, wakati akitoa salamu za chama katika hafla ya kilele cha sikuu ya wakulima kitaifa (Nanenane), zinazohitimishwa kwenye viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.

Amesema kuwa Rais Magufuli kuamua kuchukua maamuzi ya haraka na kwa wakati kwa watendaji ambao hawawajibiki kwenye maeneo ya wakuu wa mikoa hiyo, inaonyesha kuwa hawatekelezi wajibu wao.

“Kule Mwanza Juzi Rais Magufuli akiwa Wilaya ya sengerema Mkurugenzi wa Wilaya hiyo alipoulizwa bajeti ya Halmashauri alishindwa, ujumbe huu umfike Mkuu wa mkoa wa Mwanza msisubiri Rais ndiye aje kufanya maamuzi kwenye maeneo yenu,” amesema.

“Kule Morogoro Mkurugenzi alitumia kununia dawa ya mchwa kwa zaidi ya milioni 60 kinyume na utaratibu, lakini Mkuu wa Mkoa huo amekaa kimya hajachukua hatua, mpaka Rais anaamua kuchukua hatua mwenyewe na wewe Mkuu wa mkoa upo,” ameongeza Bashiru.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here