25 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

VENEZUELA KUPUNGUZA MASAA YA KAZI KUTOKANA NA KUKATIKA UMEME

Serikali ya Venezuela imetangaza kupunguza masaa ya kufanya kazi na kuzifunga shule kutokana na tatizo kubwa la kukatika kwa umeme.

Hatua hiyo imefikiwa huku rais Nicolas Maduro akitangaza mpango wa siku 30 wa kurejesha nishati hiyo.

Mpango huo utatilia mkazo upatikanaji wa maji ya kutosha kusambaza huduma hiyo.

Waziri wa Mawasiliano wa Venezuela, Jorge Rodriguez amesema kupitia kituo cha televisheni cha Serikali kuwa serikali ya Bolivia itaendelea kuzifunga shule na kupunguza masaa ya kazi hadi saa 8 za mchana kwenye ofisi za umma na binafsi ili umeme uendelee kupatikana.

Rais wa jumuiya ya wahandisi na umeme nchini humo Winton Cabas ameliambia Shirika la habari la AFP kuwa hali hiyo itaendelea na kukiri kuwa ni mbaya. Amesema, gridi ya umeme inazalisha kati ya megawati 5,500 na 6,000, ilihali uwezo wake ni megawati 34,000.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles