27.9 C
Dar es Salaam
Monday, June 24, 2024

Contact us: [email protected]

Vanessa: ‘Team’ hazisaidii chochote kwenye sanaa

VanessaNA JENNIFER ULLEMBO
KUFUATIA malumbano ya ‘team’ kwa wasanii wenye ugomvi, msanii wa muziki wa kizazi kipya, Vanessa Mdee ‘V Money’ ameibuka na kukemea makundi hayo akidai hayana faida yoyote kwa jamii na kwa sanaa za wasanii husika.
Alisema makundi hayo yanaharibu sifa ya msanii, kazi zake na yanaongeza chuki badala ya kuleta furaha na mafanikio ya msanii.
“Kama mashabiki wanapenda kazi zangu waendelee kunipenda na waonyeshe ushirikiano nami kwa wasanii wengine, lakini masuala ya timu, timu sitaki, hazina maana kwa jamii,” alisema Vanessa.
Vanessa, anayemiliki tuzo mbili za Kili, ikiwemo tuzo ya mtumbuizaji bora wa mwaka wa kike na mwimbaji bora wa kike Bongo Fleva, aliongeza kwa kuwataka wasanii walioanzisha ‘team’ waachane nazo, ili wajiongezee mashabiki badala ya kuwagawa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles