24.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, June 19, 2024

Contact us: [email protected]

Christian Bella: Kukosa tuzo kutanifanya nitoe muziki mzuri zaidi

christian bellaNA RHOBI CHACHA
MWANAMUZIKI wa Bolingo, Christian Bella, ameweka wazi kwamba kukosa kwake tuzo hata moja kutampa nguvu ya kuandaa kazi nzuri zaidi ya alizozitoa kwa mwaka jana.
Bella aliongeza kwamba, anajiamini muziki anaofanya unapendwa na wengi, kukosa tuzo hakutamrudisha nyuma bali kutamfanya aongeze nguvu zaidi ya kufanya muziki mzuri.
“Unajua mimi siku zote najijua kama nafanya kazi nzuri na mashabiki wananikubali, ila kukosa tuzo hakunivunji moyo, yaani ni sawa na kunizidishia akili ya kufanya vitu vizuri na pia nakubaliana na matokeo, hakuna tatizo lolote la kusema nilalamika, ila nawasihii mashabiki wangu wakubaliane na matokeo, wasivunjike moyo,” alifafanua Bella.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles