27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

VANESSA MDEE KUIGIZA TAMTHILIA YA MTV BASE

img_5397
Vanessa Mdee

 

NA MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

BAADA ya kumaliza mwaka na wimbo wa ‘Cashmadame’, mkali wa muziki Afrika Mashariki, Vanessa Mdee, mwakani ataanza kuonekana kwenye tamthilia ya Shuga iliyochezwa nchini Afrika Kusini.

Msimu wa tano wa tamthilia hiyo unaanza Machi mwakani ambapo Vanessa Mdee kutoka Tanzania atashirikiana na wasanii wengine kutoka nchi mbalimbali katika kunogesha msimu huo wa tamthilia hiyo.

“Nafurahi mwaka huu naumaliza vizuri na wimbo wangu wa ‘Cashmadame’ lakini mwakani Mungu akipenda nitauanza tena vyema kwa kuwa nimechaguliwa na MTV Base nishiriki katika tamthilia ya Shuga kwa msimu wa tano, ni mafanikio makubwa kwangu na kwa taifa langu na hii ndiyo itakuwa tamthilia yangu ya kwanza kuwahi kuigiza,” alieleza Vanessa.

Tamthilia hiyo anayokwenda kushiriki Vanessa ina umaarufu mkubwa kutokana na watu wengi maarufu kuwahi kushiriki, akiwamo mshindi wa tuzo ya Oscar mwaka 2014, Lupita Nyong’o kupitia filamu ya ‘Twelve Years a Slave’.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles