29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

VANESSA ATOA AHADI KWA MASHABIKI WAKE

NA CHRISTOPHER MSEKENA


 

AKIWA anajiandaa kutoa albamu yake ya kwanza (Money Mondays), nyota wa Bongo Fleva nchini, Vanessa Mdee, amewapa ahadi mashabiki ya kuendelea kufanya vizuri chini ya lebo ya Universal Music Group kwa ushirikiano na Universal Music Germany na Airforce 1.

Vanessa amesema lebo ya Universal Music Group ni kubwa duniani ina matawi ya Universal Music Africa ambayo inamsimamia Diamond Platnumz, Universal Music Europe, Universal Music America pamoja na Universal Music Central Europe anayofanya nayo kazi.

“Nimesaini dili na Universal Music Central Europe pamoja na Afrika, ndiyo maana nimesema hili ni dili la kipekee kwa kuwa nimekuwa msanii wa kwanza Afrika kusaini dili la namna hii, nimesaini mwezi wa tano na hivi karibuni mashabiki wataanza kuona kazi zangu ikiwa ni pamoja na albamu itakayotoka mwezi wa sita lakini hivi karibuni nitatoa albamu yangu ya Afrika (Money Mondays),” alisema Vanessa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles