23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

SELENA GOMEZ AMPIGA MAMA YAKE

NEW YORK, MAREKANI


MWANAMITINDO maarufu nchini Marekani, Selena Gomez, mwanzoni mwa wiki hii alimpiga mama yake kwa kosa la kuingilia uhusiano wake na Justin Bieber.

Kwa mujibu wa mitandao mbalimbali, Selena na Bieber, wamerudi kwenye uhusiano wao, lakini mama wa Selena, Mandy Teefey, hataki mrembo wake awe kwenye uhusiano na nyota huyo wa muziki wa pop. Hivyo Selena na mama yake walifikia hatua ya kurushiana maneno kabla ya kuanza kupigana huku mama huyo akidai hataki kusikia suala la Bieber.

Hata hivyo, inadaiwa kwamba mama wa Selena alikimbizwa hospitalini kufanyiwa uchunguzi, lakini siku iliyofuata aliruhusiwa kurudi nyumbani.

Kutokana na kitendo hicho, mama wa Selena ameweka wazi kuwa hana mpango wa kumshauri chochote mrembo huyo, hivyo anamwacha na maamuzi yake.

Wiki iliyopita wazazi wa Bieber walidai kuwa wanatamani kuona mrembo huyo akirudi kwenye uhusiano na mtoto wao kwa kuwa wawili hao wanaendana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles