27.7 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 21, 2024

Contact us: [email protected]

VALVERDE: MESSI SI MTU WA KAWAIDA

BARCELONA, HISPANIA

KOCHA wa klabu ya Barcelona, Ernesto Valverde, amesema kiwango alichokionesha nyota wake Lionel Messi katika mchezo wa juzi dhidi ya Espanyol, kilikuwa si cha kawaida.

Mchezaji huyo mwenye tuzo tano za mchezaji bora wa dunia wa Ballon d’Or, juzi aliisaidia timu yake kushinda mabao 5-0, huku peke yake akifunga mabao matatu.

Mabao hayo matatu yanamfanya afikishe jumla ya ‘hat trick’ 38 tangu ajiunge na kikosi hicho mwaka 2004 akiwa na umri wa miaka 13.

Valverde amedai kuwa uwezo wa Messi ni mkubwa na bado hajapata mchezaji wa kumfananisha naye katika kipindi hiki.

“Messi si mchezaji wa kawaida kama walivyo wengine, mchezo wa juzi alionesha kiwango cha hali ya juu na kuisaidia timu kuibuka na ushindi wa mabao 5-0.

“Haikuwa kazi rahisi lakini kutokana na uwezo wake binafsi aliweza kufanya mambo ya ajabu, nimekuwa na furaha kubwa kuona Messi akicheza kwa kiwango cha hali ya juu.

“Espanyol ni klabu yenye wachezaji chipukizi ambao wana uwezo mkubwa, Barcelona imekuwa na wakati mgumu ikikutana na timu hiyo, lakini safari hii imefanya makubwa,” alisema Valverde.

Mabao mengine ya Barcelona katika mchezo huo yalifungwa na nyota wake, Luis Suárez na Gerrard Peque. Hata hivyo Velverde aliongeza kwa kummwagia sifa mshambuliaji wake mpya, Ousmane Dembele ambaye aliingia na kufanya makubwa.

“Tunatarajia makubwa kutoka kwa Dembele, juzi ulikuwa mchezo wake wa kwanza na alionesha kiwango cha hali ya juu kwa muda mchache alioutumia, nina imani kubwa na mchezaji huyo katika michezo ijayo,” aliongeza.

Ushindi huo wa juzi unawafanya Barcelona wakae kileleni kwenye msimamo wa ligi, huku wakiwa na jumla ya pointi tisa baada ya kuchezo mitatu, wakati huo wapinzani wao Real Madrid wakishika nafasi ya sita wakiwa na pointi tano, baada ya kushinda mchezo mmoja na kutoka sare miwili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles