24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

NIYONZIMA AKOMAA NA CAF

Na ADAM MKWEPU-DAR ES SALAAM

KIUNGO wa Rwanda na  Simba, Haruna Niyonzima,  amesema moja ya malengo aliyojiwekea ni kuhakikisha timu hiyo inatwaa ubingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika hapo mwakani.

Simba ilikata tiketi ya kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuibuka mabingwa wa Kombe la FA msimu uliopita.

Akizungumza na MTANZANIA, kiungo huyo  aliyejiunga na Simba msimu huu akitokea Yanga, alisema ubora wa kikosi chao ndio unaomfanya aamini wana kila sababu ya kubeba taji hilo.

“Simba tuna kikosi bora msimu huu ndiyo maana nawaza ubingwa wa Afrika, naamini inawezekana kwa sababu ya aina ya wachezaji na kama tutajituma hakuna kitakachoshindikana,” alisema Niyonzima.

Niyonzima alisema licha ya ubora wa kikosi cha Simba kwa sasa, anaamini yeye binafsi ana bahati ya kuzipa mafanikio timu mbalimbali alizowahi kuzichezea tangu akiwa nchini  kwao Rwanda na baada ya kutua Tanzania.

Alisema anatambua haitakuwa kazi rahisi, lakini kiu ya mafanikio waliyokuwa nayo msimu huu anaamini itawasaidia kufikia malengo.

Hata hivyo, pamoja na kuichezea timu yake ya zamani ya Yanga kwa miaka mitano, Niyonzima hakuwahi kufanikiwa kutwaa ubingwa wowote wa michuano ya Caf.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles