26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 17, 2024

Contact us: [email protected]

UWT Sengerema waadhimisha miaka 45 ya CCM kwa kupanda miti

Na Anna Ruasha, Sengerema

Jumuia ya Wanaweke wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Sengerema mkoani Mwanza imepanda miti zaidi ya mit 200 katika kituo cha Afya Nyakalilo na eneo la ofisi ya chama hicho kata ya Nyakalilo Kama sehemu ya maadhimisho ya kuelekea miaka 45 ya kuzaliwa kwa chama hicho.

Upandaji huo wa miti umeenda sambamba na kusalimia wagonjwa na kutoa zawadi mbalimbali katika kituo cha Nyakalilo wakati Jumuiya ya wanawake wa CCM kuadhimisha kiwilaya sherehe za kuzaliwa chama hicho Februari 5, 2022 ambapo kitaifa zitafanyika mkoani Mara.

Mwenekiti wa UWT Wilaya ya Sengerema, Consitantia Faida amesema matamanio yake nikuona miti ikipandwa na kutunzwa.

“Jumui yetu imefanya maadhimisho ya kuelekea kuzaliwa kwa chama chetu kwa kufika katika kata hii lengo likiwa nikutunza mazingira, lakini pia niwaombe muendelee kumuunga mkono Rais wetu Samia Suluhu Hassan, mmeona anavyotoa fedha kwa ajili ya maendeleo na katika kituo cha afya ameleta fedha nyingi niwaombe tuendelee kumuunga mkono,” amesme Consintia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles