32.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

UWEKEZAJI MKUBWA WATANGAZWA UWANJA JULIUS NYERERE

Na Mwandishi Wetu


MAMLAKA ya Viwanja vya Ndege (TAA) imetangaza zabuni ya wazi ikiwa ni hatua ya mwanzo  kwa ajili ya uwekezaji kwa huduma mbalimbali kwenye sehemu mpya ya uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNI)   Dar es Salaam (Terminal 3).

Huduma hizo zitaufanya uwanja huo kuwa wa  pekee Afrika Mashariki, kutokana na huduma   zitakazokuwa zikitolewa kwa wasafari wanaoutumia uwanja huo.

Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa jana na TAA, wawekezaji wenye sifa wanatakiwa kupeleka maombi yao na mwisho wa kupokea maombi kwa hatua hiyo ya awali itakuwa ni mwishoni mwa Machi 2018.

Baadhi ya nafasi za uwekezaji zilizotangazwa ni pamoja ujenzi wa hoteli yenye hadhi ya nyota nne ambayo itakuwa na vyumba 200, kumbi za mikutano, casino, baa, sehemu ya maegesho ya magari na huduma nyingine muhimu.

Maeneo mengine ya uwekezaji ni ujenzi wa majengo kwa ajili ya benki , maduka kwa ajili ya kuuza bidhaa mbalimbali, sehemu za ofisi, maegesho ya magari, migahawa na sehemu za kuchezea watoto.

“Tunataraji kuwa  uwekezaji utakaofanyika utasaidia wateja wetu na abiria kuwa na chaguo la kutosha la huduma mbalimbali wakati pia ukisaidia kuongeza mapato yatakayosaidia kuboresha huduma zetu,” inasema sehemu ya tangazo hilo.

Mwishoni mwa mwaka jana, Waziri wa Ujenzi, Profesa Makame Mbarawa, alinukuliwa na vyombo vya habari akisema ujenzi wa uwanja huo wa kisasa ambao utagharimu Sh bilioni 560 utakamalika mwishoni mwa mwaka huu.

Baada ya kukamilika Terminal III, uwezo wa JNI  kuhudumia wasafiri utaongezeka na kufikia milioni sita na nusu kwa mwaka, zaidi ya mara mbili ya uwezo wa Terminal II. Terminal II ina uwezo wa kuhudumia wasafiri milini mbili na nusu kwa mwaka.

Uwanja huo pia utawezesha ndege kubwa 11 kutua kwa wakati mmoja zenye uwezo wa kubeba abiria 300 na 400, tofauti na Terminal II ambayo ina uwezo kuruhusu ndege sita tu za aina hiyo kutua kwa wakati mmoja.

Februari 8, 2017, Rais John Magufuli, alieleza kusitikishwa kwake na gharama kubwa ya ujenzi wa jengo jipya kwenye uwanja huo.

Gharama hiyo ni Sh bilioni 590  ambayo alisema ni kubwa ikilinganisha na jengo lililojengwa. Rais Magufuli alisema hayo alipofanya ziara ya kushtukiza kwenye uwanja huo.

“Hivi kulikuwa na sababu gani za nyinyi wataalamu wa serikali kukubali gharama kubwa namna hii, hivi hili jengo linafanana na bilioni 560,” aliuliza Dk. Magufuli.

Awali, mkandarasi anayejenga uwanja huo ambaye ni kampuni ya BAM International , alitangaza kusimamisha ujenzi huo kutokana na kutolipwa. Rais Magufuli aliahidi kulipa fedha hizo.

Kutokana na  hali hiyo Rais Magufuli alimuagiza Profesa Mbarawa  kuunda timu ya wataalamu watakaofanya tathimini ya utekelezaji wa mradi huo.

Alisema tathimini iwe ni pamoja na kuzungumza na mkandarasi anayejenga uwanja huo na mhandisi mshauri ambao wamekubali kupunguza gharama za ujenzi wa mradi huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles