27.6 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Uwanja wa ndege Dodoma kufanya kazi saa 24 kuanzia Oktoba mwaka huu

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa amesema mradi wa ujenzi wa taa za kuongozea ndege katika Uwanja wa ndege mkoani Dodoma uko katika hatua za mwisho ambapo unatarajiwa kukamilika Septemba 15 kabla ya kuanza kutumika rasmi Oktoba mosi mwaka huu.

Muonekano wa taa za kumuongoza Rubani kutua katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma, zikiwa zimekamilika kwa asilimia 90. Uwanja huo utaanzaa kufanya kazi usiku na mchana ifikapo mwezi Oktoba mwaka huu.

Waziri Mbarawa ameyasema hayo leo Septemba 8, 2023 jijini Dodoma alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo ambapo amesema sasa usafiri wa ndege utakuwa wa uhakika jijini humo mara baada ya maboresho hayo.

“Wote mnafahamu Dodoma ni Mji Mkuu wa Serikali, tunahitaji huduma za ndege saa 24 kila siku hivyo kwa kuweka mfumo wa taa za kuongozea ndege tutakuwa tunapata huduma za ndege saa 24 kwa siku,” amesema Waziri Mbarawa.

Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa akikagua moja ya taa za kumuwezesha Rubani Kutua usiku katika Uwanja wa ndege wa Dodoma. Maboresho hayo yanatarajia kukuamilika ifikapo Oktoba mwaka huu.

Aidha, Waziri Mbarawa amesema ili kuhakikisha huduma inakuwa ya uhakika taa hizo zimefungwa katika mfumo wa umeme wa kawaida wa Tanesco, mfumo wa jenereta pamoja na mfumo wa betri unaoweza kutunza umeme kwa saa zisizopungua nane hivyo kufanya umeme kuwa wa uhakika kila siku.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugemenzi wa huduma za Uhandsi na Ufundi kutoka Mamlaka ya Viwanja vya ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Focus Kadeghe, amesema kuchelewa kukamilika kwa wakati kwa mradi huo kumetokana na mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na vita ya Ukraine na Urusi.

Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa, akikagua maboresho na maendeleo ya mradi wa taa za kuongozea ndege uwanja wa ndege wa Dodoma. Uwanja huu unatarajia kuanza kutumika ifikapo Oktoba mwaka huu.

Pia Kadeghe amesema taa zilizowekwa zitasaidia ndege kutua hata kama kuna hali mbaya ya hewa wakati wowote huku akibainisha kuwa rubani atakuwa na uwezo wa kuziona taa hizo akiwa umbali wa takribani kilometa 25.

Kaimu Mkurugenzi Uhandisi na Huduma za Ufundi, Mhandisi Focus Kadeghe, akimuelezea Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa mfumo wa taa za kuongozea ndege katika uwanja wa ndege wa Dodoma.


- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles