23.6 C
Dar es Salaam
Saturday, May 18, 2024

Contact us: [email protected]

Changamkieni ufugaji wa samaki-Ulega

Na Esther Mnyika Mtanzania Digital

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Abdalla Ulega amewahakikishia Watanzania kuwa ufugaji wa samaki unalipa hivyo wajitokeze kwa wingi kufanya shughuli hiyo.

Kauli hiyo ameitoa leo Septemba 8, jijini Dar es Salaam jwakati akielezea fursa za uchumi wa buluu katika mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika(AGRF) Waziri huyo.

“Fursa za mifugo na uvuvi ni kubwa mno, bado tunayo nafasi ya kufanya zaidi hususani katika uvuvi wa asili kwa kuweka msukumo wa ufugaji samaki,” amesema.

Amesema serikali inafanya kila jitihada kuhakikisha uvuvi wa asili kwa kufuga samaki kwa njia ya vizimba hususani katika Ziwa Victoria.

“Serikali imeonesha njia kuwa ufugaji wa samaki unalipa kwa kuwapa boti kubwa wavuvi na hatua hiyo imewahamasisha watu wengi kuhamasika kufanya shughuli hiyo,” amesema.

Naye Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar, Suleiman Masoud Makame amesema ili kuhakikisha sekta ya uvuvi inafanya vizuri serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeanzisha sera mpya ya uchumi wa buluu na kuweka mpango mkakati wa uvuvi na kuanzisha sera ya uvuvi ya mwaka 2022.

Amesema wameweza kuwawezesha vijana kushiriki katika uvuvi na kutengeneza vikundi visivyopungua 577 kwa ajili ya uvuvi mdogo na kutengeneza boti 577 kutekeleza shughuli za uvuvi.

“Katika shughuli wa uchumi wa buluu wanayo mazao ya bahari ambayo ni mwani,ufugaji wa kaa, samaki na mazao bahari katika suala ya ufugaji tumewawesha wafanyabiashara kuwekeza katika ufugaji eneo la Unguja na Pemba,” amesema Makame.

Amesema mpango wao ni kujenga mabwawa 100 kwa ajili ya ufugaji wa mazao bahari na utekelezaji wake unaendelea na mwishoni mwa mwezi huu wanatarajia yote yatakuwa yamekamilika. Aliwataka wanaotaka kuwekeza katika uvuvi wawasili nchini kuwekeza kwa sababu kuna mazao ya bahari ya kutosha .

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles