24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Uwanja wa Bashungwa waanza kujengwa Karagwe

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Innocent Bashungwa, amewahakikishia wananchi wa Wilaya Karagwe kuwa atahakikisha anatimiza ahadi yake ya kujenga uzio na kuufanyia maboresho uwanja wa mpira wa Wilaya maarufu kwa jina la Bashungwa Stadium.

Alisema hayo Septemba 11, katika fanali ya mashindano ya Bashungwa Karagwe Cup 2022, iliyofanyika katika uwanja huo, ambao umeshaanza kujengewa msingi, ili kuwekewa uzio wa ukuta na kufanyiwa maboresho.

“Niwaahidi Wanakaragwe, itakapofika mwaka kesho katika fainali za ligi ya Bashungwa Cup, uwanja huu utakuwa umeshajengwa kwa kuzungusha ukuta na kufanyiwa maboresho na kuwa na hadhi ya uwanja wa Wilaya,” amesema Bashungwa ambaye pia ni Mbunge wa Karagwe.

Ameeleza kuwa uwanja huo wa wilaya ukijengewa uzio, utatoa fursa kwa wananchi kwa kuletwa matamasha mbalimbali na wasanii wakubwa kufanya maonesho ya muziki, ambayo yalikuwa hayafanyiki wilayani humo.

Pia Waziri Bashungwa amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kumuwezesha kutimiza ahadi yake ya kufunga taa za barabarani katika Mamlaka ya Mji mdogo wa Kayanga na Omurushaka, ambapo kazi hiyo ya ufungaji wa taa inaendelea.

Amesema ufungaji wa taa za barabarani utaendelea katika mitaa, ambapo TARURA wanaendelea na taratibu za kupata mkandarasi wa kutekeleza kazi hiyo katika mitaa ya Mji wa Kayanga na Omurushaka wilayani Karagwe.

Amesema mchakato wa ujenzi wa stendi ya kisasa ya Wilaya unaendelea, ambapo Rais Samia ameshatoa fedha, ili kukamilisha mradi huo uliosubiriwa kwa muda mrefu.

Kwa Upande Wake, Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amempongeza Waziri Bashungwa kwa kuendelea kuwatumikia kikamilifu wananchi wa jimbo hilo  na kumsaidia Rais Samia katika Wizara ya TAMISEMI.

Mashindano ya soka ya Bashungwa Karagwe Cup yanafanyika kila mwaka kwa kuzikutanisha timu za mpira za kata zote 23 za Wilaya Karagwe, ambapo mwaka huu timu ya Kata Nyabiyonza imetwaa ubigwa, ikifuatiwa na Kayanga nafasi ya pili, Kiruruma nafasi ya tatu na Chanika nafasi ya nne.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles