21.5 C
Dar es Salaam
Saturday, July 27, 2024

Contact us: [email protected]

UVCCM WATOA VIFAA HOSPITALI M’NYAMALA

Na Mwandishi Wetu-DAR ES SALAAM


UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umesema Tanzania itajengwa na Watanzania wenyewe.

Umesema suala la kupata misaada kutoka nje lisiwe kipaumbele  badala yake vijana wote wajitume kwa ajili yatTaifa lao.

Pia umoja huo  umewashukuru vijana wa Mabibo Hosteli kwa kuanzisha harambee ya kuchangia vifaa tiba  katika hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala, Mkoa wa Dar es Salaam na kuungwa mkono na umoja huo.

Msimamo huo  umetolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka alipokabidhi msaada wa vifaa vya kumsaidia mama mjamzito wakati wa kujifungua.

Vifaa vingine vilikuwa ni  kwa ajili watoto waliozaliwa chini ya miezi saba, katika Hospital ya Mwananyamala.

Alisema vijana wa CCM ndiyo wenye jukumu na wajibu wa awali wa kubuni, kuanzisha au kuibua masuala  katika kuunga mkono na kuchangia  maendeleo vijana wengine waige, kufuata na kutekeleza.

Alisema kitendo cha  kukabidhi vifaa  ni sehemu ya kukamilisha dhana ya maendeleo endelevu kwa nia ya kujenga nchi   na kumuunga mkono  Rais Dk. John Magufuli na sera za CCM katika ilani  ya mwaka 2015-2020.

“Tanzania itajengwa na Watanzania wenyewe kwa ghrama, bei yoyote.

“Natoa wito kwa makundi yote ya vijana,  kinamama na makundi mengine kujitokeza na kuunga mkono juhudi za Serikali katika nyanja zote za elimu, afya, kilimo na maeneo mengine  kuleta nguvu na msukumo wa kurahisisha maendeleo endelevu,”alisema Shaka.

Alisema wanaposema  tukutane kazi, tafsiri yake ina maana pana na mojawapo   ni ubunifu, uibuaji mipango , kuchemsha bongo na kushughulika  maendeleo ya  nchi usiku na mchana kwa vile CCM ndiyo yenye ilani na wao kama vijana ni sehemu ya utekelezaji na usimamizi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles