30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

MKE WA MUGABE ANYANG’ANYWA WALINZI

HARARE, ZIMBABWE


SERIKALI ya Zimbabwe imeondoa walinzi wa aliyekuwa Mama Taifa, Grace Mugabe huku wengi wa wasaidizi wake wakipangiwa majukumu mengine, duru zimesema.

Walinzi hao wataondolewa hatua kwa hatua hadi wiki hii, kwa mujibu wa mmoja wa maofisa waandamizi wa Serikali waliohojiwa na shirika la habari la NewsDay.

Mugabe alikuwa ametengewa walinzi kabla ya kuondolewa kutokana chama tawala cha Zanu- PF, alikokuwa akishikilia wadhifa wa uenyekiti wa kitengo cha wanawake cha chama hicho.

“Walinzi wake wanaendelea kuondolewa hatua kwa hatua,” afisa huyo ambaye hakutaka kutajwa alinukuliwa akisema.

Kutokana na hali hiyo, Grace atakuwa akitegemea kikosi cha walinzi kwa ajili ya mumewe, Rais wa zamani Robert Mugabe.

Sasa hatakuwa usemi katika utendaji kazi wa walinzi hao sababu hawatawajibika moja kwa moja kwake.

Hata hivyo, Msemaji wa Serikali, George Charamba hakuthibitisha habari hizo lakini akasema: “Kimsingi, naamini serikali haitamudu kugharamia usalama wa Chatunga (mtoto wa mwisho wa Mugabe) anapotaka kusafiri hadi Marekani au akiamua kuishi kule. Familia hiyo itakuwa ikitegemea walinzi wa Rais wa zamani.

Haya yanajiri wiki chache baada ya Rais wa Zimbabwe Emmernson Mnangangwa kuahidi kuwa atamtunza Mzee Mugabe (93) katika uhai wake.

Serikali ya Zimbabwe juzi ilichapishwa kanuni zinazoeleza stahili, ambazo marais wa zamani wanapaswa kupewa wakiwa nje ya ofisi.

Baadhi ya stahili hizo ni pamoja na walinzi, wapishi, wafanyakazi wa nyumbani, nyumba mbili, msafara wa magari na ziara nne za kimataifa kila mwaka. Stahili hizo zote zitagharamiwa kwa fedha  za walipa kodi.

Wiki iliyopita Mzee Mugabe alisafiri ng’ambo kwa ajili ya matibabu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles