26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

UVCCM Ileje kuwashughulikia wanaobeza kazi ya Rais Samia

Na Denis Sinkonde, Songwe

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UV-CCM) wilaya ya Ileje mkoani Songwe, Maoni Mbuba, amewataka vijana kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan katika kazi kubwa anayofanya.

Akifungua kikao cha baraza la kawaida la umoja wa vijana lililofanyika leo Jumatano Desemba 29, 2021, Mbuba amesema Rais Samia ametambua uhitaji wa wananchi ikiwepo sekta ya afya,elimu na maji hivyo wananchi wanapaswa kumuunga mkono ili kufanikisha azma ya Taifa.

Mbuba amesema baadhi ya wana CCM hubeza juhudi za mweshimiwa rais hivyo kama jumuiya haina budi kuisemea serikali kwa mambo inayotekeleza kuwapelekea wananchi maendeleo kwa kuzingatia Ilani ya chama cha mapinduzi.

”Wana-CCM wanapaswa kuisemea vyema serikali kwa utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika maeneo yao ikiwepo usimamizi wa ujenzi wa hospitali, vituo vua afya, miradi ya maji na ujenzi wa vyumba vya madarasa unaendelea nchi nzima ili wananchi wapate huduma hizo kwa ukaribu,” amesema Mbuba.

Baadhi ya wajumbe wa Baraza la UV-CCM wilaya ya Ileje kutoka kata 18 za wilaya hiyo wamesema hawatasita kuwachukulia hatua watu wanaobeza juhudi za Rais Samia katika kutekeleza miradi ya maendeleo.

Katibu wa chama hicho wilayani humo, Hassan Lyamba amewataka vijana hao kudumisha amani , upendo na mshikamano iliyoachwa na waasisi.

“Siasa zisiwe chanzo cha kuvunja amani, bali iwe sehemu ya kueneza amani kwa lengo la kuepusha matukio ya uhalifu hususani wilaya ya Ileje ikiwa sehemu ya nchi ya Tanzania ikipakana na nchi za Malawi na Zambia,” amesema Lyamba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles