30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Uchimbaji salama wa migodi ni ajenda ya kudumu-Dk. Biteko

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Wachimbaji wa madini wametakiwa kuzingatia uchimbaji salama katika maeneo ya migodi yao ili waweze kufanya shughuli za uchimbaji madini kwa tija na migodi iendelee kubaki salama.

Hayo yamebainishwa leo Jumatano Desemba 29, 2021 na Waziri wa Madini, Dk. Doto Biteko alipokutana na kuzungumza na wachimbaji wa madini ya dhahabu katika eneo la machimbo la Nyamalimbe Makarashani lililopo wilaya ya Geita mkoani humo.

Dk. Biteko amewaagiza wakaguzi wa migodi katika machimbo hayo kuhakikisha wanaweka utaratibu wa daftari kwa ajili ya kuhifadhi kumbukumbu kwa kusainisha majina ya wachimbaji wanaoingia na kutoka  kwenye maduara.

“Tuna watoto bado tunazaa wanahitaji madarasa, kuna akina mama wanajifunzua tunahitahitaji huduma bora za afya, maji safi, miundombinu bora na vitu vingine vingi ambavyo tunatamani vifanyike kupitia madini yetu.

“Lakini ukweli ni kwamba bado madini yetu yalikuwa hayatunufaishi kwani ukiangalia hali ya watu na sifa ya madini inayohubiriwa ni vitu viwili tofauti kwani tunao utajiri lakini unawanufaisha watu wengine na ndiyo maana Rais wetu Samia Suluhu Hassan anataka kuona utajiri huo ukibaki miongoni mwa Watanzania wenyewe,” amesema Dk. Biteko na kutoa wito kwa wachimbaji hao kusimamia kila gramu inayopatikana iende sokoni.

Aidha, katika hatua nyingine Dk. Biteko amesema Serikali inataka watu wenye leseni ya kununua madini huku akihimiza kuanzishwa kwa soko la madini katika eneo la Nyamalimbe badala ya kwenda Katoro.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles