26 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

Uturuki yawashambulia IS

Fethullah Gulen
Fethullah Gulen

ISTANBUL, UTURUKI

KWA siku ya pili mfululizo majeshi ya Uturuki yameendelea kuyashambulia maeneo ya mpakani yanayodhibitiwa na wapiganaji wa kundi lijiitalo Dola la Kiislamu (IS) nchini Syria.

Hatua hiyo ni katika kuyajibu mashambulizi yanayofanywa na kundi hilo, ikiwamo tukio la hivi karibuni la makombora mawili yaliyolenga mji wa Karkamis ulio kusini mashariki mwa Uturuki.

Mashambulizi hayo ya majeshi ya Uturuki, yalilenga maeneo manne ya mji huo yakiwamo yale ya chama cha wapiganaji wa Kikurdi cha Democratic Union.

Harakati hizo na Uturuki zinakuja siku chache baada ya IS kushutumiwa kufanya shambulizi la bomu la kujitoa mhanga katika mji wa Gaziantep ulio kusini mwa Uturuki.

Shambulizi hilo lililofanywa katika sherehe ya harusi, lilisababisha vifo vya watu 54, wengi wao wakiwa watoto na vijana wenye umri wa miaka chini ya 14 na 18.

Uturuki inakichukulia chama cha Democratic Union kuwa cha kigaidi na suala hilo pamoja na lile linalohusu mhubiri maarufu wa Kiislamu anayeishi Marekani Fethullah Gulen, ni baadhi ya yatakayotawala mazungumzo kati ya Uturuki na Makamu wa Rais wa Marekani, Joe Biden anayewasili hapa leo.

Gullen analaumiwa na Serikali ya Uturuki kwa jaribio lililoshindwa la mapinduzi ya kijeshi nchini hapa, Julai 15 mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles