27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 16, 2024

Contact us: [email protected]

Korea Kaskazini yarusha kombora Japan

Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe.
Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe.

TOKYO, JAPAN

KOREA Kaskazini kwa mara nyingine imepuuza marufuku iliyowekwa na Jumuiya ya Kimataifa baada ya kufyatua kombora kutoka kwenye nyambizi.

Jeshi la Marekani limesema kuwa lilifuatilia kombora hilo lililoruka hadi umbali wa kilomita 500 kabla ya kuanguka katika Bahari ya Japan.

Kurushwa kwa kombora hilo kumefanyika huku mawaziri wa mambo ya nje kutoka Japan, China na Korea Kusini wakiendelea na mkutano wao mjini Tokyo.

Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe, ameeleza kuwa kitendo cha Korea Kaskazini hakiwezi kukubalika, na kwamba ni tishio kwa usalama wa taifa lake.

Awali, Korea Kaskazini ilionya kuwa mazoezi ya kijeshi yanayoendelea kwa sasa kati ya wanajeshi wa Marekani na Korea Kusini yanaongeza hatari ya kuzuka vita katika rasi ya Korea.

Mazoezi hayo ambayo yamepewa jina la ‘Ulchi Freedom’, yanashirikisha wanajeshi 80,000 wa Marekani na Korea Kusini na yamejikita katika namna ya kujikinga dhidi ya uvamizi kutoka Korea Kaskazini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles